Featured Kitaifa

SHAKA AKEMEA WATENDAJI WABADHIRIFU KUFUMBIWA MACHO

Written by mzalendoeditor

Shaka akionyooshea kidole picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akimwelezea juu ya kasi ya utekelezeji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Kijiji cha Uliyankulu, Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora.

………………………………………..

Na MWANDISHI WETU, Kaliua
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka amesema Chama hiko hakiko tayari kuona wala kusikia mtendaji wa ngazi yoyote serikali aliyebainika kufanya ubadhirifu akiendelea kulelewa kwa kutochukuliwa hatua za kinidhamu.

Aidha amesema CCM haiwezi kuvumulia kuona wananchi wanyonge wakiendelea kufanywa ng’ombe wa maziwa wakati wamekuwa mstari wa mbele katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo kama ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akihamasisha.

Shaka alitoa kauli hiyo jana mbele ya wananchi wa Kijiji cha Ibambo Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora baada kusimamisha msafara wake ili kutoa kilio chao cha fedha ambayo waliichanga kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari kijijini hapo.Kwa mujibu wa wananchi hao fedha ambayo waliichanga ni Sh.995000 lakini Mtendaji waliyemtaja kwa jina moja la Mnyaga.

Akijibu malalamiko hayo ya wananchi Shaka alisema suala la kuwafanya wananchi ni ng’ombe wa maziwa hilo jambo sio sahihi kabisa na haiwezekani wananchi wanachanga fedha zao kwa ajili ya maendeleo halafu kuna na kamjanja mmoja anachukua hiyo hela kanalala nayo mbele halafu inakuwa biashara ya kawaida tu.

“Hiyo ni sahihi ndugu zangu? Huko ni kurudishana nyuma , huko ni kukwamishana, kuumizana.Sasa sisi kama Chama tumeshamueleza Mkuu wa Wilaya na tunamsisitiza kwa sababu hilo jambo tunalo, huyu mtu amekula hizo fedha za wananchi na baada ya kula hizo fedha ofisi ya Mkurugenzi ikamhamisha ikampeleka kijiji kingine ili kusudi akaendeleze huo ubadhirifu.

“Yaani ameharibu sehemu moja amechukuliwa akaharubu sehemu nyingine, akaumize wananchi wa chini kabisa, hiyo ni haki? Kama amekula fedha za wananchi mmejiridhisha na wananchi wenyewe wanalalamika, mnaondoa tatizo sehemu moja mnapeleka sehemu nyingine.

“Kwa bahati mbaya ofisi ya Mkurugenzi nayo inalaumia kwamba inalea uozo na taarifa tulizonazo ofisi ya mkurugenzi inalaumiwa inalea watendaji ambao ni wabadhirifu , na tunayo orodha ya watendaji ambao ni wabadhirifu kwenye halmashauri hii , watendaj wa vijiji na kata imekuwa ndio tabia yao.Chama Cha Mapinduzi hakiwezi kuvumilia wananchi wanyonge wanyonywe halafu baadhi ya viongozi waendelee kuwalea wanyonyaji,sio sahihi,”alisema Shaka

Alifafafanua kuwa sio dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akihamasisha wanannchi kufanya kazi nao kuitikia kwa vitendo kuona wananyonywa na kuwekewa mazingira magumu ya kufanikisha miradi ya maendeleo.

Alisema inashanga kuona wananchi wanachanga fedha Sh.995000 halafu anatokea mjanja mmoja anachukua fedha hizo na kisha anaondoka zake.“Hata Rais Samia haungi mkono hicho kitu , kwa hiyo ofisi ya Mkurugenzi na ninyi pia mnayo matatizo , kwasababu haiwezekani kulea uozo huu .

“Haiwezekani sisi tunakuja wananchi wanasema jamani sisi fedha zimeliwa na ndio kumekwamisha hata matundu ya vyoo kujengwa.Kumbe wakwamisha wa maendeleo wako hapa hapa.CCM hatuwezi kulea watu wa aina hii.

“Rais Samia halali mmemsikia wakati anaapisha wakuu wa mikoa,Rais halali kwa kufikiria namna gani atawakwamua Watanzania lakini leo kuna wasaidizi wake wako huku chini wanamhujumu, Chama hiki hakiwezi kuvumilia,”alifafanua Shaka.

Aliongeza anaomba huyo Mtendaji afuatwe huko aliko na kisha alipe fedha aliyochukua na kwamba lazima vitendo hivyo vikome halafu kuna watu wanakaa wanasema eti Serikali hii inawavumilia wabadhirifu,

“Serikali CCM inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan haitamvumilia mbadhirifu yoyote awe kwenye kijiji, kitongoji, Kata ,Wilaya, halmashauri, Mkoa au awe Taifani.Na Rais alishasema mkitaka kujua rangi halisia chezea fedha za umma

“Kabla ya kuondoka kwenye huu mkoa wa Tabora nisikie hatua zimechukuliwa na tunamfuatilia na mimi nimeanza kumfutilia tangu nimetoka Dar es Salaam,”alisema Shaka na kusisitiza orodha ya watendaji wabadhirifu wanayo na wanaanza na mtendaji huo, lazima kieleweke.

MIFUMO UTOAJI FEDHA SERIKALINI

Katika hatua nyingine Shaka alisema kuwa wanafuatilia mifumo ya utoaji fedha ya Serikali ambayo inadaiwa kuwa chanzo cha kukwamisha miradi ya maendeleo

Shaka alisema mfumo usiwe kisingizio cha kukwamisha shughuli za maendeleo za wananchi, msitumie mfumo kama kisingizo cha urasimu kukwamisha shughuli za wananchi

“Tunakwenda kufuatilia tuambiwe shida nini, haiwezekani mfumo mwezi mzima haufunguki? Hawa ukiwaambia mfumo haufunguki watakuelewa lakini mimi sikweli, kwa sababu kwanza siamini humo mfumo mwezi mzima usifunguke, siamini hata siku moja, sasa tutakwenda kufuatilia kwa nini kumekuwa na urasimu wa masuala muhimu na ya msingi yanayogusa maisha ya wananchi hawa.

“Na huo urasimu unatokana na huo mfumo kwamba mwezi mzima haufunguki au unatokana na nini? Na kama ni urasimu wa mfumo tutashauriana na Serikali kuboresha mifumo yake ili kuendana na kasi na spidi ya maendeleo ya Rais Samia Suluhu Hassan, nimemsikia Waziri wa fedha juzi wakati anasaini mikata ya tarura mbele ya rais, alisema Rais anapotoa fedha zikachelewa kutoka Rais anafutilia mara kwa mara sasa kule juu rais anafuatilia huku chini tunataka kuona ufuatiliaji wa karibu ili mikwamo hii iwe inakwamuka na wananchi wafaidike na miradi ya maendeleo inayotolewa na Rais Samia Suluhu Haasan ambayo inawagusa wao moja kwa moja.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ( ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, (katikati) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Tabora kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 mkoani humo, kushoto ni mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Batilda Burian na kulia ni Solomon Kasaba. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, (katikati) akizungumza na wananchi katika kiniwe cha kahawa Lumumba, mjini Tabora.

Shaka akionyooshea kidole picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, wakati akimwelezea juu ya kasi ya utekelezeji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Kijiji cha Uliyankulu, Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora.

Shaka na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Gilbert Kalima, wakishiriki ujenzi wa kituo cha Afya Mwongozo kilichopo Kata ya Mwo,ngozo, wilayani Kaliua Mkoa wa Tabora.

Shaka akizungumza na Wana CCM na wananchi katika Shiba Namba 5, Kijiji cha Uliyankulu, Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025.

About the author

mzalendoeditor