Featured Michezo

KMC FC YAWASILI SALAMA ARUSHA KUWAKABILI COAST, POLISI TANZANIA

Written by mzalendoeditor

Kikosi cha Timu ya KMC FC chenye wachezaji 24 kimewasili salama Jijini Arusha kwa ajili ya michezo miwili ya Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania bara itakayopigwa Agosti 17 na 21 katika uwanja wa Sheih Amri Abeid Jijini hapa.

KMC itakuwa Jijini hapa ambapo siku ya Jumatano ya Agosti 17 itashuka katika Dimba hilo dhidi ya Coast Union ya mkoani Tanga na Jumapili ya Agosti 21 utakuwa ni mchezo wa pili dhidi ya Polisi Tanzania na kwamba katika michezo hiyo yote miwili itakuwa ugenini.

Awali kwa mujibuwa ratiba ya Bodi ya Ligi kuu Tanzania (TPLB) ilipanga michezo hiyo miwili dhidi ya Coast kupigwa katika uwanja wa Mkwawani Tanga huku ule dhidi ya Polisi Tanzania ungepigwa katika uwanja wa ushirika Moshi lakini kutokana na taarifa ya kufungiwa kwa viwanja hivyo ikapeleka kupangwa katika uwanja wa Sheih Amri Abedi.

Katika msafara huo KMC imewaacha wachezaji wa tatu ambao ni Blase Bigirimana, Waziri Junior pamoja na Eric Manyama ambapo sababu za kutosafiri na Timu kwa wachezaji hao ni nikutokana na kuwa majeruhi ambayo waliyapata wakati wa mazoezi.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya Kocha Mkuu Thierry Hitimana imejiandaa kikamilifu katika michezo hiyo miwili ambayo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kwamba kila Timu imejiandaa ipasavyo hivyo mipango na mikakati kama klabu ni kuhakikisha kuwa inapata matokeo mazuri kwenye michezo hiyo ya mwanzo wa Ligi.

“Tumekuja kutafuta alama sita muhimu kwenye michzo hii miwili, tunafahamu ushindani mkubwa utakavyokuwa kwenye michezo hii , lakini kama Timu tunapokwenda kuanza ligi tunahitaji ushindi jambo ambalo linawezekana kwakuwa michezo yote ipo ndani ya uwezo wetu”.

Kwa upande wa Afya za wachezaji wote wako vizuri na kila mmoja anamorali na hari ya kuhakikisha kuwa Timu inapata matokeo ambayo mashabiki na Watanzania wote wanataka kufurahi, tunawaheshimu wapinzani wetu lakini ushindi kwetu ni kipaumbele cha kwanza.

About the author

mzalendoeditor