Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS), Francis Kiwanga (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.9 ikiwa ni ruzuku kwa baadhi ya Asasi za Kiraia (AZAKI) kati ya 89 za Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na azaki hizo hafla iliyofanyika leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.
…………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
SHIRIKA la Foundation for Civil Society (FCS), limetoa ruzuku ya Sh.Bilioni nne kwa Asasi za Kiraia (AZAKI) 89 kwa Tanzania bara na visiwani ili kutekeleza miradi ya kimaendeleo chini ya program ya utawala bora katika sekta za maji,elimu afya na kilimo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga,wakati wa warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI hizo zilizochaguliwa kupata kati ya 1,200 zilizoomba.
Amesemwa kuwa FCS imejikita katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa inawasaidia wananchi katika kuboresha maisha maisha yao na kukuza sekta ya asasi za kiraia.
“Tumepata wadau 89 wanaotoka mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar na kazi kubwa itakayofanyika ni kusukuma ajenda ya utawala bora hapa nchini,”amesema.
Bw.Kiwanga amesema kuwa eneo jingine la utawala bora ni vita dhidi ya kuondoa ukatili wa kijinsia lakini pia kundi la vijana, kuhakikisha rasilimali zinazotolewa na serikali na wadau wengine, kweli ziwafikie makundi hayo na watu wenye mahitaji maalum.
Pia katika sekta za elimu, afya na kilimo, usawa wa kijinsia, ujumuishwaji wa vijana na watu wenye ulemavu, na ujenzi wa amani na mshikamamo wa kijamii kwa mwaka 2022-2023.
“FCS imepitisha mpango mkakati mpya wa mwaka 2022-2026 ambao unataka kuona wananchi waliowezeshwa, wastahimilivu, wanaowajibika na wanaopata haki za kiuchumi, kijamii na kuboresha ubora wa maisha yao.
Kiwanga amesema kuwa kumekuwepo ongezeko la migogoro katika rasilimali hivyo kwa sasa kuna taasisi 10 zitafanya kazi ya kuitatua hususani maeneo ya Kusini, Morogoro na Kilosa.
Amesema FCS imeweka mfumo madhubuti wa kuhakikisha kila shilingi inatumika kwa lengo lilokusudiwa huku taasisi zizofuata utaratibu watachukua hatua kali.
Kwa upande wake ,Meneja Programu Utawala Bora FCS, Edna Chilimo amesema FCS wanafanya kazi na mashirikia madogo ambao ni wabia na viongozi wa klasta za programu wambao wanafanya kazi katika ngazi ya taifa.
Amesema wanafanya kazi na asasi za kijiji, kata na wilayani huku wabia ni mashirika tunayofadhili ni wadau muhimu.
Chilimo amesema mashirika yanayofadhiliwa na FCS sio waruzukiwa tu, ni wabia pia na kwamba baadhi ya misingi ya ubia ni uelewa wa pamoja,malengo ya pamoja, na kuaminiana ili kuweza kufikia malengo ya pamoja.
“Tumekuwa walezi wa sekta ya AZAKI, tumechangia ukuaji wa sekta, miaka ya nyuma tulitoa fedha kwa Azaki kujisajili na sasa kuna Azaki zimekua, kutoka shirika dogo hadi kuwa mashirika makubwa yenye sifa,”amesema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la TAWSEI kutoka Mkoa wa Tanga, Bernadethe Choma,amesema wao kama NGO’S kupitia ruzuku wanazopewa zitaenda kuboresha maisha ya wakazi wa maeneo husika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS),Francis Kiwanga,akizungumza wakati wa warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI 89 zilizochaguliwa kupata kati ya 1,200 zilizoomba leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS),Francis Kiwanga,akisisitiza jambo kwa washir8iki wa warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI 89 zilizochaguliwa kupata kati ya 1,200 zilizoomba leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS),Francis Kiwanga,(hayupo pichani) wakati wa warsha ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI 89 zilizochaguliwa kupata kati ya 1,200 zilizoomba leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Foundation for Civil Society (FCS), Francis Kiwanga (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.9 ikiwa ni ruzuku kwa baadhi ya Asasi za Kiraia (AZAKI) kati ya 89 za Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na azaki hizo hafla iliyofanyika leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.
BAADHI ya waliokabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.9 ikiwa ni ruzuku kwa baadhi ya Asasi za Kiraia (AZAKI) kati ya 89 za Tanzania Bara na Zanzibar kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na azaki hizo wakionyesha mikataba ya utekelezaji wa ruzuku hiyo leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.
Meneja Programu Utawala Bora FCS, Edna Chilimo,akielezea jinsi fedha zitakazofanya kazi katika jamii mara baadhi ya Asasi za Kiraia (AZAKI) kati ya 89 za Tanzania Bara na Zanzibar kukabidhiwa bilioni 4 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na azaki hizo wakionyesha mikataba ya utekelezaji wa ruzuku hiyo leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la TAWSEI kutoka Mkoa wa Tanga, Bernadethe Choma,akizungumza mara baada ya kuwa mmoja wapo wa asasi za kiraia zitakazo pokea ruzuku za FCS kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa na azaki hizo wakionyesha mikataba ya utekelezaji wa ruzuku hiyo leo Agosti 15,2022 jijini Dodoma.