Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akizungumza na viongozi pamoja na wananchi waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,ameitaka TARURA kutoa orodha ya makandarasi waliowahi kuharibu ujenzi wa miundombinu ili wasipewe kazi huku akionya tabia ya kuwepo kwa madalali wanaotoa zabuni kwa watu wasio na uwezo wala sifa.
Rais Samia ametoa agizo hilo wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 ambapo leo imesainiwa mikataba 10 kati ya 960 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
RAIS Samia ameitaka TARURA kutowapa mikataba baadhi ya wakandarasi ambao ni wababaishaji ili kuepuka kuisababishia hasara Serikali .
”Naagiza Mikataba yote 960 iende kwa wakandarasi wenyewe hasa wa ndani na kujiepusha na madalali ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na kwa kuchelewa na kubainisha kuwa wakandarasi wababaishaji hawatakuwa na nafasi.”amesema Rais Samia
Aidha amewataka wakandarasi wazawa kubadilika na kujenga barabara za kudumu na zenye kutumia teknolojia japo kwa miaka 10 badala ya mazoea ya ujenzi wa barabara za msimu zinazoisababishia serikali gharama za mara kwa mara.
RAIS Samia ameelekeza ofisi ya Mwanasheria Mkuu kushirikiana na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia vifungu vya kisheria kuhusu teknolojia ya ujenzi wa barabara na madaraja nchini ili kuongeza tija na thamani ya fedha katika miradi ya barabara nchini.
“Huko nyuma kila mwaka mabilioni yalikuwa yanatolewa kurekebisha barabara, mvua zikija zinabomoa. Hata hivyo, Kuna teknolojia mbadala tuzitumie hasa maeneo ya vijijini ili barabara zikijengwa kuwe na nafasi ya angalau miaka saba ndio tufanye matengenezo.”
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 ujenzi wa barabara kwa Kiwango cha lami utakua na urefu wa km 422, Kiwango cha changarawe urefu wa km 11,074, Madaraja 269 na Matengenezo kwa barabara yatakayofanyika ni ya urefu wa km 21,595.
Bashungwa amesema bajeti ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara vijijini na mijini imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 272.56 mwaka 2020/21 hadi Shilingi bilioni 722 katika mwaka wa fedha 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 185.
”Mwaka wa fedha 2022/23 ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati ambapo TARURA imetengewa bajeti ya jumla ya Shilingi bilioni 838.16 ambapo kati ya hizo Shilingi bilioni 776.63 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 61.53 ni fedha za nje.”
Amesema Ofisi ya Rais-TAMISEMI ilitoa maelekezo kwa TARURA kuanza taratibu za manunuzi mapema ili kazi ziweze kuanza kabla ya kipindi cha mvua ambapo tayali TARURA ilitangaza zabuni 1,085 zenye thamani ya Shilingi bilioni 378.56, sawa na asilimia 60% ya fedha zilizopangwa kutekeleza miradi ya barabara za vijijini na mijini, kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Bashungwa amesema mpaka sasa miradi iliyotayari kusainiwa ni mikataba 968, yenye thamani ya Shilingi bilioni 248.74, na miradi yenye thamani ya Shilingi bilioni 129.83, imetangazwa upya baada ya Wakandarasi walioomba kutokidhi vigezo.
Hata hivyo Waziri Bashungwa ametoa wito kwa Makandarasi wanapofanya kazi katika maeneo mbalimbali katika halmashauri kutimiza jukumu lao la kulipa kodi husika (Service Levy) na wanapoandaa zabuni zao wakumbuke sehemu ya kodi ambazo huchangia kwenye mapato ya halmashauri zinazopaswa kulipwa.
Naye Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amesema kuanzia mwaka 2021/22 hadi 2026/27 lengo ni kuongeza mtandao wa barabara za lami kwa km 1,450.75 kutoka km 2,404.90 zilizopo hivi hadi kufukia Km 3,855.65, changarawe km 73,241.57 kutoka km 29,116.57 hadi kufikia km 102,358.14 na madaraja 3,808 kutoka 2,812 hadi kufikia madaraja 6,620.
Aidha amebainisha kuwa fedha zitakazotumika kwenye mpango huu zinakadiriwa kuwa zaidi ya Shilingi trilioni 4.2.
‘Mpango Mkakati wetu wa pili ni kuwa ifikapo 2026/27 asilimia 85 ya mtandao wa barabara za Wilaya chini ya TARURA zitakuwa zinapitika kwa misimu yote na nyakati za mvua hapatakuwa na taharuki inayojitokeza sasa kwa maeneo mengi kujifunga.”amesema Mhandisi Seff
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akishuhudia utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akizungumza na viongozi pamoja na wananchi waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI ,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe Mwigulu Nchemba,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff,akitoa taarifa ya utekelezaji wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe,akitambulisha Viongozi kwa makundi mbalimbali waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala na Serikali za Mitaa (USEMI) Mhe.Abdallah Chaurembo,akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
Mkandarasi aliyepata tenda Mhandisi Maina Waziri,akizungumza kwa niaba ya wakandarasi wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
WABUNGE wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
VIONGOZI ,Wakandarasi pamoja na wananchi wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushuhudia utiaji saini Mikataba Kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Makandarasi watakaotekeleza kazi za Ujenzi,Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya Barabara kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 iliyofanyika leo Agosti 14,2022 jijini Dodoma.