Featured Michezo

DKT. MPANGO APONGEZA CRDB BANK MARATHON KUKUSANYA SHILINGI BILIONI 1.05 KUSAIDIA JAMII

Written by mzalendoeditor
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiongoza mbio za hisani za CRDB Bank Marathon maalum kwaajili ya kusaidia watoto wenye magonjwa ya moyo na wakina mama wenye ujauzito hatarishi zilizofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 14 Agosti 2022.(Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete Naibu Spika wa Bunge Mheshimiwa Mussa Zungu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji CRDB Bank Abdulmajid Nsekela. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Pauline Gekuli).
**********************
‘Wakimbiaji waondoka na zawadi zaidi ya shilingi milioni 100’
Na mwandishi wetu
 Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ametoa pongezi kwa mbio za hisani za kimataifa zinazoandaliwa na Benki ya CRDB “CRDB Bank Marathon” kwa ku”kisha lengo la kukusanya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kusaidia jamii.
Dkt. Mpango ametoa pongezi hizo wakati akikabidhi mfano wa hundi kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya na Hospitali ya CCBRT muda mchache baada ya kukamilika kwa mbio hizo ambazo zilishirikisha zaidi ya wakimbiaji 6,200.
Alipongeza uamuzi wa Benki ya CRDB kuendelea kusaidia upasuaji wa watoto wenye magonjwa ya moyo, pamoja na wazo jipya la kusaidia upatikanaji wa huduma salama za uzazi kwa wakinamama wenye ujauzito hatarishi alibainisha.
“Afya ya mama na mtoto ni moja ya maeneo yanayopewa kipaumbele kikubwa katika Sera ya Afya. Ninafarijika kuona mbio hizi zinasaidia kuimarisha eneo hili kwa kufanikisha upatikanaji wa huduma ya matibabu kwa watoto na wakinamama,” aliongezea.
Dkt. Mpango alisema fedha hizo zilizokusanywa zitasaidia kupunguza makali ya gharama kwa ajili ya upasuaji wa moyo na huduma za uzazi kwa wakinamama wenye ujauzito  hatarishi ambazo watu wengi hawawezi kuzimudu pamoja na Serikali kutoa ruzuku ya asilimia 80.
Dkt. Mpango alisema Serikali inaunga mkono na kufurahishwa sana na ubunifu wa taasisi za kizalendo kama Benki ya CRDB kusaidia sekta za kijamii kama vile afya, elimu, mazingira, na uwezeshaji kwa vijana na wanawake.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiongoza mbio za hisani za CRDB Bank Marathon maalum kwaajili ya kusaidia watoto wenye magonjwa ya moyo na wakina mama wenye ujauzito hatarishi zilizofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 14 Agosti 2022.(Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete Naibu Spika wa Bunge Mheshimiwa Mussa Zungu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji CRDB Bank Abdulmajid Nsekela. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Pauline Gekuli).Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na washiriki wa mbio za hisani za CRDB Bank Marathon maalum kwaajili ya kusaidia watoto wenye magonjwa ya moyo na wakina mama wenye ujauzito hatarishi zilizofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 14 Agosti 2022.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Brenda Msangi mfano wa hundi ya shilingi milioni 220 zilizopatikana kutokana na mbio za hisani za CRDB Bank Marathon maalum kwaajili ya kusaidia watoto wenye magonjwa ya moyo na wakina mama wenye ujauzito hatarishi zilizofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 14 Agosti 2022.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete  Dkt. Delilah Kimambo mfano wa hundi ya shilingi milioni 250 zilizopatikana kutokana na mbio za hisani za CRDB Bank Marathon maalum kwaajili ya kusaidia watoto wenye magonjwa ya moyo na wakina mama wenye ujauzito hatarishi zilizofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 14 Agosti 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea medali ya kumaliza kilometa 5 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya CRDB Dkt. Ally Laay wakati wa kuhitimisha mbio za hisani za CRDB Bank Marathon maalum kwaajili ya kusaidia watoto wenye magonjwa ya moyo na wakina mama wenye ujauzito hatarishi zilizofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 14 Agosti 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na washindi mbalimbali wa mbio za hisani za CRDB Bank Marathon maalum kwaajili ya kusaidia watoto wenye magonjwa ya moyo na wakina mama wenye ujauzito hatarishi zilizofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 14 Agosti 2022. Kushoto kwa Makamu wa Rais ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji CRDB Bank Abdulmajid Nsekela.

About the author

mzalendoeditor