Featured Kitaifa

WIZARA YA MAJI YAENDELEA NA UTEKELEZAJI WA KUKAMILISHA UJENZI NA UPANUZI WA MIRADI INAYOENDELEA

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin-DODOMA

WIZARA ya Maji imeidhinishwa jumla ya shilingi 709,361,607,000 kwaajili ya matumizi na kati ya fedha hizo, matumizi ya kawaida ni shilingi 51,462,269,000 ambapo shilingi 16,700,534,000 ni kwaajili ya kugharamia matumizi mengineyo.

Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi akizungumza na Waandishi wa habari leo 12 Agusti, 2022 Jijini Dodoma
Amesema Wizara ya Maji inasimamia sekta Muhimu inayohusu uhai wa binadamu na viumbe hai wengine

“Sote tunajua kwamba bila Maji hakuna uhai hivyo utekelezaji wa shughuli zozote zinazolenga kuboresha uwepo wa Maji, upatikanaji wake kwa matumizi mbalimbali pamoja na ubora stahiki ni kipaumbele cha kudumu kwenye mikakati ya Wizara na Serikali kwa ujumla”, amesema

“Vipaumbele vya Wizara kwa Mwaka 2022 na 2023 ni pamoja na kukamilisha ujenzi, ukarabati na upanuzi wa Miradi uayoendelea kutekelezwa kuanzia ujenzi wa mabwawa ya kimkakati ya Kidunda na Farkwa, na kuanzia ujenzi wa Miradi ya maji mipya ikiwemo Miradi ya Maji katika Miji 28”.Amesema Mahundi

Aidha amesema Rasilimali za mani zilizopo Nchini zinakadiriwa kuwa mita za ujazo bilioni 126 kwa Mwaka zikiwemo bilioni 105 juu ya ardhi na bilioni 21 chini ya ardhi.

“Serikali katika Mwaka 2022 na 2023 itaendelea kuwekeza katika utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuboresha ufanisi katika matumizi ya Maji kwa lengo la kuepusha nchi kuwa na uhaba wa Maji”, amesema

” Lakini pia Usimamizi na ubora wa Maji ni moja walo ya masuala muhimu katika maendeleo ya Taifa letu katika kukinda afya ya Jamii,mazingira na vyanzo vya Maji”. Amesema Mahundi

Ameongezea kwa kusema kuwa upatikanaji wa huduma ya Majisafi na salama kwa Wananchi waishio Vijijini inafikia zaidi ya asilimia 85.

“Ifikapo 2025 Wizara imepanga kutekeleza jumla ya miradi 1029 ya Maji ambapo miradi 648 ni miradi inayoendelea kutekelezwa na miradi 381 ni mipya”,amesema

“Utekelezaji wa Miradi hiyo inategemewa kuounguza adha ya upatikanaji wa Maji kwa Wananchi,kuongeza ajira na kupunguza gharama za matibabu kutokana na magonjwa yanayohusiana na Maji”. Amesema Mahundi

Wizara imepanga kutekeleza jumla ya Miradi 175 yenye kulenga kuboresha upatikanaji wa Majisafi na salama kwa Wananchi waishio Mjini na utekelezaji huo ni sehemu ya kufikia zaidi ya asilimia 95 ya upatikanaji wa Maji katika maeneo ya Mjini ifikapo Mwaka 2025.

About the author

mzalendoeditor