Featured Kitaifa

PESA ZA MAENDELEO ZA RAIS SAMIA HAIJAWAHI KUTOKEA TANGU UHURU – MBUNGE DEO SANGA

Written by mzalendoeditor

Mbunge wa Jimbo la Makambako mkoani Njombe, Deo Sanga, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka pesa za maendeleo kila kona ya nchi.

Sanga amesema kuwa uwekezaji huo wa serikali ya Rais Samia kwenye miradi ya maendeleo haujawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru.

 

Mbunge huyo, maarufu kama Jah People, aliongea wakati wa mkutano wa hadhara kwenye ziara ya Rais Samia mkoani Njombe, huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

 

“Awamu ya 6 imemwaga mahela mengi ya maendeleo haijapata kutokea tangu nimekuwa seneta (Mbunge) wa Bunge hili Haki ya Mungu,” alisema Sanga huku akitikisika mwili.

 

“Zimemwagika hela za maendeleo mpaka natizama nasema Mama (Rais Samia) Mungu akujaalie sana.”,amesema.

 

Sanga pia ni Mwenyekiti wa Wabunge wa mkoa wa Njombe na Mwenyekiti mstaafu wa CCM mikoa ya Iringa na Njombe.

 

Amesisitiza kuwa uwekezaji huo wa serikali ya Rais Samia kwenye miradi ya maendeleo sekta za afya, elimu, maji, barabara, umeme na miundombinu mingine “haujapata kutokea” tangu nchi ipate uhuru.

 

“Miradi tuliyoipata, tumepata mabilioni na mabilioni na mabilioni,” alisema.

 

Mbunge wa Njombe Mjini, Deodatus Mwanyika, naye aliipongeza serikali ya Rais Samia kwa kuwekeza pesa nyingi kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi.

About the author

mzalendoeditor