Featured Kitaifa

DAR, TABORA MOTO MKALI UMISSETA

Written by mzalendoeditor

 

Asila Twaha, Tabora

Mashindano ya UMISSETA yanayoendelea Mkoa wa Tabora yemekuwa na mpambano mkali kwa kila mechi kutaka kuutwaa ubingwa wa UMISSETA 2022, kwa timu kuonesha makali katika uchezaji.

Hayo yamedhihirika leo katika mpambano uliochezwa asubuhi kati ya timu ya Dar es Salaam mpira wa kikapu na Kigoma ambapo Dar es Salaam imecheza kwa kiwango cha juu na kumpiga mpinzani wake timu ya Kigoma pointi 79-10.

Kwa muonekano wa washangiliaji wa upande wa Dar es Salaam kuonekana na nyuso za furaha kwa kusema na kuwapa nguvu wachezaji wao kwa kuwashangilia.

“Mazoezi yaendelee, mazoezi yaendelee” washangiliaji Dar es Salaam.

Vilevile kwa upande wa timu ya mpira wa wavu wasichana Tabora yajinyakulia seti 3-0 kwa jumla(overall performance) kwa kuwashinda wapinzani wao timu ya Dodoma katika mechi iliyochezwa asubuhi ya leo viwanja vya Tabora Wavulana.

Awali timu ya Tabora na Dodoma kuoneshana ubabe kwa kutofautiana 29-19 seti, 25-21 seti na 25-18 seti na baadae timu ya Tabora kuondoka na seti 3-0 kwa jumla na kuwafanya kuibuka na ushindi.

Naye Kapteni wa Timu ya Dodoma mpira wa wavu Jacline Athony amesema, pamoja na kushindwa kwao lakini wanaendelea kujipanga kuhakikisha mechi inayofuata wanashinda.

“Nitoe wito kwa wachezaji wenzangu pointi za kwenye ubao zinavyoandikwa zisitupanikishe sisi niwachezaji wazuri tutulie uwanjani ili tushinde” Jackline

Mashindano ya UMISSETA ni ushirikiano wa wanafunzi wa Shule za Sekondari kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

About the author

mzalendoeditor