Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AAGIZA MADIWANI NJOMBE KUSIMAMIA MAPATO

Written by mzalendoeditor
NJOMBE 
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza madiwani kwenda kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao ili fedha ziweze kuwaletea maendeleo wananchi. 
Akiwa mjini Makambako mkoani Njombe wakati akielekea mkoani Iringa Rais Samia amesema ni lazima madiwani wasimamie mapato ya ndani kikamilifu na kudhibiti upotevu ili kuwasaidia wananchi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofanyika katika maeneo yao. 
Waziri wa Uwekezaji viwanda na biashara Ashatu Kijaji amesema ili kuongeza fursa za kiuchumi kwa watanzania serikali inakwenda kuanza uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe mchuchuma na chuma cha liganga wilayani ludewa mkoani Njombe baada ya mchakato wa kuwatafuta wawekezaji sahihi kufanyika. 
Awali mbunge wa Makambako Deo Sanga amemuomba Rais kumsaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo kuchelewa kuwalipa fidia wananchi waliotwaliwa eneo lao na jeshi la polisi pamoja na kumsaidia kuongeza miradi ya maji licha ya fedha nyingi za maji alizotoa. 
Juma Aweso ni waziri wa maji ambaye anakiri kuwapo kwa upungufu wa lita milioni tano za maji mjini Makambako ambazo zimeshapatiwa fedha.
Rais Samia Suluhu Hassan amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Njombe na kuwaaga wananchi akiwa Makambako ambapo hivi sasa ameanza ziara hiyo katika mkoa wa Iringa.

About the author

mzalendoeditor