Featured Kitaifa

CHANGAMOTO YA MAFUTA NCHINI YAIFANYA ALIZETI KUWA ZAO LA KIMKAKATI

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin- Dodoma

MTAALAMU wa kilimo Jeshi la Magereza Nzuguni Mkoani Dodoma Salum Mohamed, amesema Serikali imeamua kufanya zao la alizeti kuwa zao la kimkakati kutokana naTanzania kuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa mafuta.

Akizungumza na Mzalendo blog Agosti 10, 2022 Jijini Dodoma
amesema zao la alizeti linafaida nyingi tikiachana na kuzalisha mafuta lakini pia unaweza kuzalisha kitu kingine tofauti na mafuta.

“Tanzania kumekuwa na changamoto kubwa sana ya upatikanaji wa mafuta na ndiomaana Serikali imefanya maamuzi mazuri kufanya zao la alizeti kuwa zao la kimkakati ,na zao la alizeti linafaida nyingi tukiachana na upatikanaji wa mafuta kwasababu alizet majani yake unaweza kutumia kama chakula cha mifugo kama sungura lakini pia makapi yake ukitoka kukamulia mafuta yanaliwa na kuku pamoja na Ng’ombe”,amesema

“Na zao la alizeti sisi kama magereza tumejipanga kimkakati kulilima katika magereza mengi hasa katika ukanda wa kati kwasababu ndio sehemu ambayo inastawi sana kwasababu zao hili la alizeti halihitaji mvua nyingi”.Amesema Mohamed

Ameongezea kwa kusema Mavuno bora utokana na mbegu bora hivyo wao wanazingatia mbegu bora na urutubisho wa ardhi kwasababu hii itawasaidia katiza uzalishaji mzuri wa mbegu na mazao bora.

” Sisi tunazingatia wakati sahihi wa kupanda zao la alizeti na pia tunazingatia sana urutubishaji wa ardhi kwa kupanda mbegu zenye ubora na wakulima tunapaswa kulima kilimo hai ili kunufaika zaidi

“Kingine cha kuzingatia kwa wakulima hasa katika zao hili la alizeti ambalo ni zao la kimkakati limepewa kipaumbela katika Nchi yetu katika zao la alizeti ni kudhibiti wadudu wanao shambulia zao la alizeti”.Amesema Mohamed

About the author

mzalendoeditor