Featured Kitaifa

WANANCHI WAENDELEA KUILILIA SERIKALI JUU YA UPANDAJI WA GESI

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin-DODOMA

Baadhi ya Wananchi wa Nzuguni Mkoa wa Dodoma wameiomba Serikali kuondoa vikwazo ambavyo vinasababisha kupanda kwa mafuta na kupelekea pia kupanda kwa gesi.

Anna Mathias Akizungumza na Mzalendo blog Leo 8 Agosti, 2022 katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati ikiwa na kauli mbiu isemayo “Agenda 10/30 kilimo ni biashara, shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo mifugo na uvuvi”Jijini Dodoma.

“Sijajua mahusiano ya Mafuta na gesi ila tunaona kwamba mafuta yakipanda na gesi nayo inapanda na sahivi kila kampuni gasi ni Tsh.24 mpaka Tsh.25

“Tumejaza tu mitungi ndani haina chochote, Serikali itufikirie kwaili kwasababu gesi inaturahisishia mambo mkaa unatuchosha”.Smesema Mathias

Naye Antony Juma Msambazaji wa gesi za Taifa Gas pamoja na amesema Mafuta na gesi ni kitu kimoja hivyo pale ambapo mafuta yanapanda na gesi nayo inapanda na inatokana na gesi nyingi zinatoka huko nje ya Nchi hasa katika maeneo na Ukraine na Urusi.

“Gesi nyingi zinapatikana huko nje kwaio kadri mafuta yanapopanda bei na mafuta nayo yanapanda hasa katika kipindi hichi ambacho kumekuwa ma machafuko ambayo yanaendelea kati ya Urusi na Ukraine.

” Gesi ni zao la Mafuta na gesi imeanza kupanda tangu mwezi wa Nne kutoka Tsh.22 mpaka Tsh.24 na hii kutokana na bei ya mafuta kupanda.

Ameongezea kwa kusema katikati ya wiki hii yawezekana pia gesi kupanda kutokana na bei ya mafuta kupanda kuanzia Tsh.3500 na gesi inategemea pia kupanda na hii inatokana na gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa.

“Hili kusambaza gesi kwa wateja ni lazima utumie usafiri ambao unatumia mafuta kwaio hii nayo inapelekea gesi kupanda kwa kasi

“Na kipindi cha nyuma tulikuwa tunauza kwa bei nafu kuanzia Tsh.18500 mpaka Tsh.22 kwaio sisi tunaendana na Mafuta, Mafuta yakipanda na gesi nayo inapanda mara mbili ya mafuta.

About the author

mzalendoeditor