Featured Michezo

VIGOGO WA SOKA NCHINI SIMBA,YANGA KUANZA UGENINI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Written by mzalendoeditor

YANGA watacheza mchezo wao wa awali kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini ambapo Mshindi wa mchezo huo atacheza na mshindi kati ya St. George ya Ethiopia dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Simba watacheza na Big Bullet ya Malawi katika mchezo wa awali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wataanzia ugenini huku mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi kati ya Red Arrows ya Zambia dhidi ya Premiro Agosto ya Angola.

Huku wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Geita FC wataanzia ugenini dhidi ya Bilal Al Sahil ya Sudan kwenye hatua ya awali huku Azam FC wao wakianzia hatua ya kwanza  watacheza na mshindi kati Al Akhder v Al Ahli Khartoum.

About the author

mzalendoeditor