Featured Michezo

KMC FC YATAJA KIKOSI CHAKE CHA MSIMU WA 2022/23

Written by mzalendoeditor

Klabu ya KMC FC kuelekea katika msimu mpya wa 2022/2023 itakuwa na jumla ya kikosi cha wachezaji 27 ambapo kati yao maingizo mapya ni 14 huku wale waliokuwa kwenye mpango wa kocha Mkuu Thierry Hitimana mara baada ya kumalizika kwa msimu wa 2021/2022 ni 13.

wachezaji waliosajiliwa wapya ni pamoja na George Makang’a, Ibrahim Ame, Baraka Majogoro, Isaac Kachwele, Styve Nzigamasabo, Blaise Bigirimana, Boniphace Maganga, Daruweshi Saliboko, Waziri Junior, David Kisu, Nourdine Balora, Erick Costantine, Farshad Mogela pamoja na Balisi Maliki.

Kwa upande wa wachezaji wazamani waliobakizwa na Timu ni Matheo Anthon, Kelvin Kijiri, Klifu Buyoya, Masoud Kabaye, Mohamed Samata, Sadallah Lipangile, Ismail Gambo, Abdull Hillary, Emmanuel Mvuyekule, Awesu Ally Awesu, Andrew Vicent, Kenny Ally Mwambungu pamoja na  Hance Masudi.

Benchi la ufundi msimu huu KMC haijafanya mabadiliko na kwamba litabaki kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo Kocha Mkuu amebaki Hitimana huku akisaidiwa na Ahmad Ally, Emmanuel Kingu kocha wa Magolikipa pamoja na Faraji Muya meneja wa Timu.

Aidha Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni inaendelea na maandalizi ya msimu mpya ambapo Agosti 17 itashuka katika Dimba la Mkwakwani mkoani Tanga kuwakabili Coast Union mchezo ambao utakuwa ni wa kwanza kwa msimu wa 2022/2023 kwa KMC ugenini.

“Tunafahamu msimu wa 2022/2023 utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kwamba kila Timu imejiandaa kiushindani, lakini siku zote Manispaa ya Kinondoni imekuwa ikihakikisha inafanya vizuri kwenye michezo yake na kwamba malengo makubwa ni kumaliza katika nafasi Nne za Juu jambo ambalo lipondani ya uwezo wetu.

 “Ukiangalia msimu huu tunaidadi kubwa ya maingizo mapya ya wachezaji ambao wote wanauzoefu wa kucheza ligi ya Tanzania nan je ya Nchi,  hivyo katika kujenga muunganiko wa wachezaji jambo hilo linakwenda vizuri na hivyo ni watoe hofu mashabiki kuwa tunatimu nzuri na bora yenye ushindani kuelekea kuanza kwa msimu mpya Agosti 17 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

About the author

mzalendoeditor