Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo akizungumza na wateja wa benki hiyo mkoa wa Kigoma wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Maofisa wa Benki ya Exim wakiongozwa na Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo (katikati) waliosimama wakizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Kigoma iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda akizungumza na wateja wa benki hiyo mkoa wa Kigoma wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo (kulia) akijipongeza na baadahi ya wateja wa benki hiyo mkoa wa Kigoma wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakipata chakula wakati wa hafla hiyo
Maofisa wa Benki ya Exim wakiongozwa na Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo (wa pili kushoto walioketi) na Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda (wa pili kulia walioketi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Kigoma iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
…………………………….
Na Mwandishi Wetu-Kigoma
BENKI ya Exim Tanzania imejipanga kutumia vema uwepo wake mkoani Kigoma kuchochea ukuaji wa biashara baina ya Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda na Burundi kwa kuboresha zaidi huduma zake ikiwemo mikopo ya biashara na kilimo sambamba na kuwajengea uwezo zaidi wajasiriamali katika mkoa huo.
Akizungumza kwenye hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake mkoani Kigoma, Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa benki hiyo, Andrew Lyimo alisema jiografia ya mkoa wa Kigoma inatoa fursa zaidi kwa wafanyabiashara mkoani humo kunufiaka zaidi na fursa za kibiashara baina ya Tanzania na mataifa jirani ya jirani ya Kongo, Rwanda na Burundi.
“Hata hivyo ili wafanyabishara hawa waweze kunufaika kikamilifu na fursa hii ya kijiografia ni vema sana kwa sisi kama taasisi za kifedha kuona kwamba tuna jukumu kubwa la kuwasaidia kufanikisha hilo kwa kuhakikisha kwamba si tu tunawapatia huduma za kifedha bali pia tunawejengea uwezo kwa kuwapatia elimu kuhusu biashara na ujasirimali kisha ndipo tuwapatie mikopo ili wakashindane vema na wenzao kutoka mataifa jirani,’’ alisema.
Alisema benki hiyo imekuwa ikitumia ipasavyo hafla hizo za jioni na wateja wake katika kubadilishana ujuzi na fursa baina yake na wateja hao ili waweze kunufiaka vema na huduma za benki hiyo zilizobuniwa kuendana na uhalisia wa mahitaji ya wateja wake.
“Mbali na hafla hizi za jioni maofisa wetu wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tunawasaidia wateja kwa kuwajengea uelewa zaidi kuhusu mbinu za kutafuta masoko, mbinu za kujenga mtandao wa kibiashara (Business network) lakini pia tunawapa uelewa wa namna ya kuandaa maandiko yao kwa ajili ya kuomba mikopo,’’ alisema.
Awali wakizungumza kwenye hiyo, Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda pamoja na Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo walisema benki kwa sasa inauweka mkoa wa Kigoma katika vipaumbele vyake kwa kuhakikisha zaidi huduma zake katika mkoa huo zinakwenda sambamba na mkakati wa mapinduzi ya kiuchumi ya mkoa huo.
“Tumebaini kwamba kwasasa mkoa wa Kigoma unapitia mabadiliko makubwa ya kiuchumi katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara na kilimo ambayo yanahitaji ushiriki mkubwa wa taasisi za kifedha na hivyo benki ya Exim tupo tayari kwa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha hilo. Ujio wa huduma yetu ya Exim Wakala unalenga kufanisha hilo zaidi hivyo tunaomba sana wana Kigoma mtupokee,’’ alisema Bi Kaganda.
Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria hafla hiyo walielezea namna wanavyolizishwa na huduma zinazotolewa na benki hiyo huku wakitumia fursa hiyo kuiomba taasisi hizi izidi kujitanua zaidi mkoani humo pamoja na kanda nzima ya Magharibi pamoja na nchi jirani ili waweze kunufaika zaidi na huduma zake zinazotolewa kidigitali zaidi.
“Ndio maana leo tumeshukuru sana kuona Benki ya Exim imetuita hapa kututangazia kwamba ipo pamoja na sisi katika kufanikisha hili. Tunawashukuru sana kwa hilo na sisi tupo tayari kuendelea kushirikiana nao ’’ alisema Bw Issa Athumani mmoja wa wafanyabiashara mkoani humo.