Kitaifa

WAZIRI MKENDA AUTAKA UONGOZI WILAYANI RUNGWE KUTENGA ENEO MAPEMA KWA AJILI YA UJENZI WA VETA

Written by mzalendoeditor

 

Na Mathias Canal, Kiwira-Mbeya

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda ameutaka uongozi wa Wilaya ya Rungwe kutafuta eneo la zaidi ya Hekari 20 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa chuo cha ufundi stadi-VETA.

Waziri Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 7 Agosti 2022 alipopewa fursa ya kujibu hoja zilizoibuka wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Wilayani Rungwe ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mbeya iliyoanza tarehe 5 Agosti 2022 hadi tarehe 8 Agosti 2022.

Waziri Mkenda amesema kuwa Katika bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2022/2023 zimetengwa Bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa Vyuo vya Ufundi stadi-VETA katika wilaya mbalimbali nchini hivyo Wilaya ya Rungwe ni mojawapo katika mpango huo.

About the author

mzalendoeditor