Featured Kitaifa

WATENDAJI WA VIJIJI WASAIDIE MATUNZO KWA WAZEE: MPANJU

Written by mzalendoeditor

 

Na WMJJWM, Mtwara

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amesema watendaji wa vijiji ni muhimu kuhakikisha wazee wanatunzwa ili kuipunguzia Serikali gharama ya kuwatunza katika makazi.

Mpanju ameyasema hayo Agosti 06, 2022 alipotembelea kijiji cha Mkaseka, Wilaya ya Masasi mkoa wa Mtwara katika Makazi ya Wazee yaliyofungwa na Serikali baada ya kuwarudisha wazee hao kwenye familia zao.

Awali Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mkaseka Thabit Bakari alieleza kuwa baada ya makazi hayo kufungwa wazee walirudishwa kwenye jamii na yeye kama mtendaji anawafuatilia.

Kwa upande wake mmoja wa wazee hao waliorudi kijijini Cosmas Mbedo amesema yupo tayari kuendelea kukaa kijijini ambako anapata huduma mbalimbali kutoka kwa wanajamii.

Akizungumza ofisini kwake, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Abdallah Malela amewataka maafisa Maendeleo ya Jamii kuwa wabunifu ili kuisaidia jamii kukabiliana na changamoto zilizopo ndani ya jamii ikiwemo makundi ya wazee na watoto.

About the author

mzalendoeditor