TANZANIA imetupwa nje kwenye kinyang’anyiro cha tiketi ya Fainali za Soka la Ufukweni Afrika licha ya ushindi wa 7-6 jioni ya leo ufukwe wa Coco Jijini Dar es Salaam.
Malawi inafuzu kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya 9-9 kufuatia ushindi wa 3-2 kwenye mchezo wa kwanza nyumbani.