Featured Kitaifa

WAZIRI GWAJIMA AIPONGEZA MONTESSORI KWA MFUMO BORA WA ELIMU 

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Dkt. Dorothy Gwajima akikagua mabanda ya maonesho ya kazi za Jumuiya ya Montessori wakati wa maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo Agosti 3,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25, ya jumuiya ya Montessori Tanzania (MCT) yaliyofanyika leo Agosti 3,2022 jijini Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25, ya jumuiya ya Montessori Tanzania (MCT) yaliyofanyika leo Agosti 3,2022 jijini Dodoma.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii Msaidizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Baraka Makona akitoa salaam za Wizara kwaniaba ya Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25, ya jumuiya ya Montessori Tanzania (MCT) yaliyofanyika leo Agosti 3,2022 jijini Dodoma.

MKUU wa Montessori Community of Tanzania (MCT) Sr.Denise Mattle,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25, ya jumuiya ya Montessori Tanzania (MCT) yaliyofanyika leo Agosti 3,2022 jijini Dodoma.

MENEJA Mradi kutoka Uswis Benjamin Brühwiler,akielezea namna wanavyoendelea kusaidia Montessori wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25, ya jumuiya ya Montessori Tanzania (MCT) yaliyofanyika leo Agosti 3,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori Community of Tanzania (MCT) Bi.Sarah Kiteleja,akizungumza wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25, ya jumuiya ya Montessori Tanzania (MCT) yaliyofanyika leo Agosti 3,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Amina Mfaki, akitoa salaam za Ofisi hiyo wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25, ya jumuiya ya Montessori Tanzania (MCT) yaliyofanyika leo Agosti 3,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Dkt. Dorothy Gwajima,akikabidhi tuzo mbalimbali kwa washiriki mara baada ya kufungua  maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25, ya jumuiya ya Montessori Tanzania (MCT) yaliyofanyika leo Agosti 3,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Dkt. Dorothy Gwajima,akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori Community of Tanzania (MCT) Bi.Sarah Kiteleja mara baada ya kufungua  maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25, ya jumuiya ya Montessori Tanzania (MCT) yaliyofanyika leo Agosti 3,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha na washiriki mara baada ya kufungua  maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25, ya jumuiya ya Montessori Tanzania (MCT) yaliyofanyika leo Agosti 3,2022 jijini Dodoma.

………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amefurahishwa na Mfumo wa Elimu unaotolewa na Taasisi ya Montassori huku akizitaka Jumuiya hizo za Montessori kuwafikia watoto wa Hali zote katika jamii ili kuwapatia fursa ya kupata Elimu ya Awali kwani Elimu hiyo ni ya muhimu sana kwa ufahamu wa Mtoto.

Hayo ameyasema leo Agosti 3,2022 jijini Dodomma wakati akifungua maadhimisho ya Jubilee ya miaka 25, ya jumuiya ya Montessori Tanzania (MCT).

Dkt. Gwajima,  ameipongeza Jumuiya hiyo kwa juhudi zao za kuwapatia watoto Elimu ya Awali inayowawezesha watoto kuwa na udadisi , utambuzi binafsi na kujiamini ba kuwaepusha na ukatili wa aina yoyote.

“Ajenda yangu ya kwanza baada ya Sensa ya watu na Makazi ni kufanya harambee ya ujenzi shirikishi wa vituo vya watoto na kuchukua mbinu ya Montessori ili watoto wengi wanufaike hasa wa pembezoni na hata wale wenye mahitaji Maalum” Alisema Dkt. Gwajima.”

Akizungumza wakati wa Maadhimisho hayo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii Msaidizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Baraka Makona amesema hatua zilizochukuliwa za urahisishaji wa leseni ya kuendesha Vituo vya Malezi itasaidia wadau kuanzisha Vituo vingi vitakavyowezesha kutoa huduma ya Malezi na elimu ya Awali kwa watoto wengi nchini.

“Upatikanaji wa Leseni umerahisishwa na kuwa ndani ya siku tatu hivyo nawasihi mlete maombi ya Leseni za vituo ili viweze kusajiliwa na Watoto wengi waweze kufaidika zaidi” amesema Makona

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Montessori Martha Dello amesema Vitendo vya ukatili vinatokana na malezi duni na kukosekana kwa Malezi imara kwa watoto hivyo Taasisi yao inashirikiana na Serikali kuhakikisha watoto wanapata sehemu nzuri za kupata Malezi Makuzi na Maendeleo yao ya Awali kwa ustawi wa Watoto na jamii.

“Vitu haviibuki tu tukiwa watu wazima, ni msingi kutoka utotoni, kuna vitendo vingi vya ukatili kwa sababu ule msingi wa kwanza ulikuwa umeharibika,n ndiyo maana pamoja adhabu nyingi bado vinaendelea” alisema Martha.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Mtoto (TECDEN) Mwajuma Rwebangira alisisitiza juu ya umuhimu wa Malezi ya Awali kwa watoto kwani ni hatua mhiku katika ukuaji wa Mtoto kwani ndio inamjenga katika kuwa Rai mwema na mwenye uzalendo na taifa lake.

“Tuendeleze Ajenda ya mtoto ya malezi kwani inawajengea watoto uwezo wa kubaini mambo mbalimbali ya msingi katika umri Mdogo hivyo kuwarahisishia maisha” alisema Bi. Mwajuma

Akitoa Salamu za Ofisi ya Rais TAMISEMI Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Amina Mfaki amesema mbinu za Montessori zimekuwa zikitumika katika kuwaeilimisha watoto wa Tanzania kwa miaka 55 hivyo Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kuweka mifumo mizuri ya kuhakikisha watoto kuanzia Elimu ya Awali wanapata Malezi bora hivyo kuwa na Taifa lenye raia wenye kujitambua, kuwajibika na uzalendo kwa Taifa lao.

About the author

mzalendoeditor