Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU AAGIZA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUWAWEZESHA VIJANA NCHINI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako,akitembelea Vibanda kwa niaba ya Waziri Mkuu Majaliwa wakati wa  hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022) iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako,akizungumza  kwa niaba ya Waziri Mkuu Majaliwa wakati wa  hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022) iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako,akizungumza  kwa niaba ya Waziri Mkuu Majaliwa wakati wa hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022) iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la USAID, V.Kate Somvongisiri,akizungumzia mradi ulivyowanufaisha vijana wakati wa hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022) iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mkurugenzi  wa utawala kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI  Victor Kategere,akitoa maelekezo ya utangulizi wakati wa hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022) iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022)  kwa niaba ya Waziri Mkuu Majaliwa iliyofanyika leo Julai 27,2022 jijini Dodoma.

……………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ameagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha zinawatambua na kuendelea kutoa mikopo ya Vijana kupitia Mikopo ya asilimia kumi ili kuendeleza juhudi zilizoonyeshwa na wadau wa Maendeleo nchini.

Agizo hilo lilitolewa leo Julai 27,2022 jijini Dodoma  na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako wakati  akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Majaliwa kwenye hafla ya kufunga mradi wa Feed the Future Tanzania Inua Vijana uliotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani(USAID) kwa miaka mitano (2017-2022).

Prof.Ndalichako amesema kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika maendeleo ya vijana na maeneo mengine yenye lengo la kuleta usawi kwa wananchi.

”Vijana ni nguzo na rasilimali muhimu katika Taifa hivyo Serikali imekuwa ikuchukua hatua  za kuhakikisha kwamba inaleta ustawi kwa vijana  na kuweka  Mazingira wezeshi ya kuweza  kupata maendeleo, hivyo kila Halmashauri inawajibu wa kutenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha vijana kichumi kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu.”amesema Prof.Ndalichako

Prof. Ndalichako ameiagiza Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) kushirikiana na  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kuhakikisha Vijana wanaedelea kuwezeshwa kwa kujengewe uwezo na kupewa vitendea kazi ili waweze kujikwamu kiuchumi Na kuleta maendeleo nchini
Aidha, Prof. Ndalichako amezitaka Wizara na Taasisi zote zinazohusiana na ustawi wa jamii kushirikiana kwa pamoja kwa kuweka Mpango Mkakati wa kushughulika changamoto zinazoakabili vijana wa makundi yote nchini. 

” Tunashukuru Shirika la USAID lakini tunaomba kuangalia namna ya kupanua programu hii ifike kwenye mikoa mingine zaidi ya hii ya awamu ya kwanza,”amesema

Awali, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la USAID, V.Kate Somvongisiri amesema Programu hiyo imehusisha vijana wa vijijini wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 kujihusisha na biashara ya kilimo na minyororo mingine ya thamani na kuongeza fursa zao za kiuchumi huku wakikuza uongozi na maisha bora.
” Tunajivunia kuwa mradi huu Inua Vijana umewafikia zaidi ya vijana 43,000 na kutoa zaidi ya shilingi bilioni 5.3 (dola za Marekani milioni 2.3) kama ruzuku kwa biashara na kilimo zinazomilikiwa na vijana.”amesema Somvongisiri
Kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amewataka vijana walionufaika na programu ya Feed the Future kutumia mafunzo hayo kuzalisha na kupiga hatua na kuleta faida kwa jamii inayowazunguka.
Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mkurugenzi  wa utawala kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI  Victor Kategere amelishukuru shirika  la Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani,USAID Tanzania kwa kuwainua vijana kiuchumi na kuwapongeza Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zilizonufaika na mradi huo kwa usimamizi uliotukuka.

About the author

mzalendoeditor