RAIS wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini,(TUCTA),Tumaini Nyamhokya,akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 27,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu kuwasilisha Mapendekezo yao ya Nyongeza ya Mashahara kwa Serikali.
………………………………..
Na Eva Godwin-DODOMA
SHIRIKISHO la vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kimewasilisha mapendekezo yao serikalini kuhusu kiwango cha nyongeza ya mishahara kwa Watumishi wa Umma ili kiangaliwe Upya huku wakisisitiza hawajaridhishwa na kiwango cha nyongeza kilichoongezwa cha mishahara watumishi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 27,2022 jijini Dodoma Rais wa chama hicho Tumaini Nyamhokya,amesema kuwa wamesilisha mapendekezo hayo kwa Katibu Mkuu , Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora.
Amesema Vyama hivyo vimewasilisha mapendekezo yake serikalini kupitia ofisi ya Rais manajementi ya utumishi wa umma na utawala bora ili serikali iangalie upya nyongeza ya mishahara kwani kuna baadhi ya kada hazikupata nyongeza ya mishahara.
“Mambo ya msingi ambayo tumeyazingatia ni namna ya nyongeza ya mshahara unavyofanyika ambapo haikumridhisha mtumishi yoyote amepata nyongeza hiyo kwasababu tumeona kiwango cha nyongeza ni cha chini sana”,amesema
“Na tukumbuke Mh.Rais alilenga kuongeza mishahara na hakuwa amelenga kuwatoa watu daraja fulani kuwapeleka sehemu fulani,kwaio tunaamini kama ni nyongeza ya mshahara inagusa kila Mshahara wa Mtumishi wa Umma”.amesema
Nyamhokya
Katika hatua nyingine TNyamhokya ameomba nyongeza ya mishahara itazamwe kwa kuangalia asilimia na sio kiwango cha mshahara wa Mtu huku akisisitiza kila mtumishi anahaki ya kupata mshahara mzuri kulingana na kazi yake.
“Kuna baadhi ya taasisi za umma hazikuguswa kwa mfano kuna watumishi wengi wenye mishahara binafsi na wamegawanyika kuna wale wa darasa la saba ndio hawakuguswa kwasababu wanasema hawasomeki kwenye Mfumo wa Serikali, na wale viongozi wa kata Pamoja na viongozi wa Mtaa”,amesema
“Kwaio tumeona kumekuwa na ubaguzi mkubwa na sababu hatuoni ni nini ambayo inafanya ngazi nyingine za mshahara zisiguswe
Lakini kuna baadhi ya Taasisi pia tumejaribu kuchunguza hazijaguswa kabisa na nyongeza kama TTCL,ATCL pamoja na Taasisi nyingine nyingi”.Amesema Nyamhokya
Ameongezea kwa kusema kiwango cha elfu70 sio kiwango halisia cha kumtoa mtumishi kwenye maisha ya ghali katika kipindi hiki cha hali ya uchumi kuwa chini Nchini.