WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,akiendelea na ukaguzi katika soko la wamachinga linalojengwa Jijini Dodoma leo Julai 26,2022 mara baada ya kufanya ziara yake.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,akitoa maelezo kwa wasimamizi wa ujenzi wa Soko la wamachinga linalojengwa Jijini Dodoma leo Julai 26,2022 wakati wa ziara yake.
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,akizungumza mara baada ya kufanya ziara katika soko la wamachinga linalojengwa Jijini Dodoma leo Julai 26,2022 .
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,ya kukagua soko la wamachinga linalojengwa Jijini Dodoma leo Julai 26,2022 .
MWAKILISHI wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Dickson Kimaro,akipokea maagizo ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo,mara baada ya kutembelea soko la wamachinga linalojengwa Jijini Dodoma leo Julai 26,2022 .
………………………….
Na Eva Godwin-DODOMA
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt.Seleman Jafo amewataka TPDC kufunga mtambo mkubwa wa gesi katika soko kubwa la wamachinga jijini Dodoma ambalo lipo katika hatua ya mwisho ya ujenzi
Ameyasema hayo Julai 26,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake ya kutembelea Soko hilo kubwa la Wamachinga lililopo Bahi road ambapo lipo katika hatua ya mwisho ya ujenzi Jijini Dodoma
Amesema soko hilo ni la kisasa Jijini Dodoma hivyo lazima kywe na mitambo ya kisasa itakayowasaidia wamachinga kufanya biashara zao
“hili ni soko la kisasa kwaio nilazima kwa watu hawa wanaofanya biashara ya upishi kupika vyakula katika soko nilzama kujali mazingira ,wanapaswa kujali ajenda ya mazingira kwaajili ya kutumia gesi”,amesema
“Tunatakiwa tuwe na mfumo mmoja hapa wa Natural gas hili watu watumie kuweka mfumo Mmoja tu wa kulipa bili kuliko kila mmoja kuweka mtungi wake na hii sio nzuri katika suala la biashara”.Amesema Jafo
Ameongezea kwa kusema Soko hilo ni la Mfano Tanzania nzima hivyo amemtaka Mkurugenzi Wa Jiji kusimamia suala hilo la Mfumo wa Natural Gas kupatikana katika soko hilo kwa kufanya mawasiliano na Mtendaji Mkuu wa TPDC kufanya utaratibu wa kupata Natural Gas.
“Nakuagiza Mkurugenzi wetu wa Jiji fanya mawasiliano ma Mtendaji Mkuu wa TPDC kuwa tuna soko la kisasa ambalo ni la mfano Tanzania , mueleze tunataka soko hili tupate utaratibu mzima wa kupata Natural Gas”,amesema
“Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi tuna utajiri mkubwa wa gesi kwaio hili suala naomba lifikishwe kwa TPDC japo tutaanza na mitungi ya kawaida ya Gesi huku tukiwa tunawasubiri TPDC “.Amesema Jafo
Dk.Jafo amesema soko hilo ni lazima liwe na Mtu muhimu wa kusimamia suala zima la mazingira kwa kufanya soko liwe na muonekano mzuri,
sambamba na yote hayo amempongeza Mkandarasi wa soko hilo kwa kufanya kazi vizuri katika kusimamia ujenzi wa soko hilo
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema soko hilo linatarajiwa kukamilika ifikapo Agusti Mwaka huu ambapo ametoa wito kwa Vijana wanaofanya kazi za umachinga kuwa maandaliza yanaanza ya kuwapanga zaidi ya machinga 6000 kuingia ndani ya soko hivyo amewataka baadhi ya Wamachinga ambao hawajajiandikisha majina yao wafike katika ofisi ya jiji kuweka majina yao.
“Tumeanza utaratibu wa kuwapanga Wamachinga, na zaidi ya machinga 6000 wataingia humu ndani hatuitaji Machinga wengine wabaki huko na tumezingatia Wamachinga wote kwaio fikeni katika ofisi za jiji kuandikisha majina yenu,
Mradi huu ni mradi wa machinga katika Mkoa wa Dodoma na tunawaona sahivi wanavyopata tabu katika biashara zao na umebaki mda mchache tu soko hili kukamilika
“Na nimesikia kuna maneno yanaendelea kuwa vibanda vingi humu ndani ni vya watu wa Serikalini niwaambie tu kuwa hakuna kibanda cha Mtu wa serikalini humi, vibanda vyote ni vya wamachinga tena wa hali ya chini”.Amesema Mtaka