TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Caroline Kitana Chipeta kuwa Balozi wa Tanzania, The Hague nchini Uholanzi.
Balozi Chipeta alikuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Uteuzi huu unaanza mara moja.