Featured Kitaifa

SAFARI YA UFUNDISHAJI LUGHA YA KISWAHILI NCHINI AFRIKA YA KUSINI YAANZA

Written by mzalendoeditor

Wataalamu wa elimumsingi ikiwemo mitaala, elimu ya ualimu, mitihani kutoka nchini Afrika Kusini wamewasili nchini leo Julai 25, 2022 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa Hati ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika ya Kusini katika maeneo mbalimbali ya elimumsingi ikiwemo kubadilishana wataalamu wa kufundisha na kujifunza Lugha ya Kiswahili.

Jopo hilo limepokelewa na Mwenyeji wake Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolonia Bibi Sylvia Lupembe kwa kushirikiana na wataalam wa Tanzania wanatarajiwa kuandaa mpango kazi wa utekelezaji

About the author

mzalendoeditor