Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki katika Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kwa ajili ya Heshima ya Wimbo wa Taifa wakati ukipigwa kwenye Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka silaha za jadi (Ngao na Mkuki) kwenye mnara wa Mashujaa kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi kwenye Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka wakati akiondoka katika viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma
…………………………………..
Na Eva Godwin-DODOMA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan amependekeza kutafuta eneo kubwa zaidi ya kujenga Mnara wa Mashujaa zaidi wenye hadhi ya kishujaa.
Ameyasema hayo leo Julai 25,2022 katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa Tanzania ambapo kitaifa imefanyika Jijini Dodoma.
Amesema Jiji la Dodoma ndio Makao makuu ya Nchi hivyo anamtaka Mkuu wa mkoa wa Dodoma pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu kutafuta eneo kubwa la kujenga Mnara wenye hadhi ya kishujaa ili kuwaeshimisha zaidi mashuja wetu wa Tanzania.
“Napendekeza kutafutwa kwa eneo kubwa lenye hadhi kubwa ambapo utajengwa mnara mkubwa zaidi wa huu na niseme kwamba kamati ya maandalizi mmenitahidi sana katika kusimamia suala hili la siku ya mashujaa kwenda vizuri”
“Mkuu wa Mkoa wa Dodoma najua pia utalisimamia suala hili la kutafuta eneo kubwa zaidi kwaajili ya kujenga mnara wenye hadhi ya kishujaa”.Amesema Suluhu
Ameongezea kwa kusema Maadhimisho haya sio kwa Mashujaa ambao hawapo duniani ila ni kwa wote ambao wapo hai na ambao hawapo hai, waliopata ulema wa kudumu katika kupigania Taifa la Tanzania na ambao ni wazima wa Afya.
“Siku hii ya Mashujaa ni Muhimu kwa Mashujaa wetu wote na waliopo Duniani na ambao hatupo nao Duniani
“Wapo Mashujaa ambao walipigana kwaajili ya Taifa letu wakapata Ulemavu wa kudumu na leo hii pia ni siku yao”.Amesema Suluhu