Featured Kitaifa

WAZIRI GWAJIMA AKOSHWA NA NGUVU YA TLS KUPAMBANA NA VITENDO VYA UKATILI

Written by mzalendoeditor

Na WMJJWM, Dar es Salaam.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima, amefurahishwa na Chama cha Mawakili nchini (Tanganyika Law Society- TLS) jinsi walivyo mstari wa mbele katika kuibua na kufuatilia matatizo ya jamii ikiwemo ukatili wa kijinsia na kwa watoto ndani ya jamii.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo katika mdahalo juu ya Visa vya Mauaji katika mahusiano ya kimapenzi nchini Tanzania uliofanyika Julai, 23, 2022 Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Chama cha Mawakili (TLS) ni wa kuigwa mfano kama walivyo wadau wengine wanaokerwa na ukatili kwa kuona ukubwa wa tatizo hata kuamua kufanya mdahalo huo ambao itasaidia kuibua changamoto za kupambana na vitendo vya ukatili na njia zaidi ya kupambana na vitendo hivyo.

“Ni wazi kuwa kama kuna mtu au Kikundi cha watu bado hakijafahamu ukubwa wa tatizo la ukatili basi ni dhahiri watashindwa kulinda vizazi vyetu” alisema Waziri Gwajima.

Aidha, Dkt. Gwajima ameiteuwa TLS kuongoza Kamati ya Jamii ya Ushauri kuhusu kupambana kutokomeza Ukatili.

Kwa upande wake Rais wa TLS nchini Prof. Edward Hosseah amesema kuwa ombi lao ni kuwa na Mtaala wa Malezi utakaozingatia elimu ya mapokeo lakini kwa kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.

“Tumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuunda Wizara hiyo na kumteuwa Dkt Dkt Gwajima kuiongoza” alisisitiza Prof. Hossea.

Kwa upande wake Mchungaji Mstaafu wa KKKT Mchlungaji Richard Hananja aoisema tatizo lililopo ndani ya Jamii ni Ukombozi wa fikra ambazo zimesababisha Jamii kuingia katika janga kubwa na zito la vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo Jamii ikikombolewa kifikra na kuamua kuamka na kupambana na vitendo hivyo, Jamii itakuwa sehemu salama yanjuisjinhasa kwa watoto na Wanawake amabo wamekuwa waathirika wakubwa wa vitendo hivyo.

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu Anna Henga alisema kwa sasa hali ya ukatili imekithiri kwani kati ya wanandoa 10, sita kati yao wanapitia ukatili hivyo aliiomba jamii kubadili mitazamo kwani unyanyasajj hauna maana kwa maendeleo na Ustawi wa Jamii.

Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Mary Kafyome aliomba kuundwa kwa kikosi kazi kwa ajili ya kusukuma ajenda hiyo ya kukomesha ukatili kitakachojumuisha wanajamii wenyewe kwani vitendo vya ukatili vinatokea kwa wingi katika jamii hasa nyumbani na katika Shule na hata Vyuo Vikuu.

About the author

mzalendoeditor