Featured Michezo

MATUKIO KATIKA PICHA:YANGA WAKIENDELEA NA MAZOEZI YA MSIMU WA 2022/23 AVIC TOWN

Written by mzalendoeditor

Mchezaji Mpya wa Yanga beki kutoka DR.Congo Joyce Lomalisa Mutambala kiendelea na mazoezi katika viwanja vya Avic Town Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Wachezaji Zawadi Mauya pamoja na Golikipa Eric Johora wakijifua kwa ajili ya mashindano mbalimbali Msimu wa 2022/23.

Wachezaji Abdallah Shaibu Ninja pamoja Benki mwenzake kutoka Zanzibar beki Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’ 

Mchezaji Mpya kutoka Zambia Mshambuliaji Lazarous Kambole akiwa na mshambuliaji mwenzake Yusuph Athumani wakiendelea kujifua vikali.

Mchezaji Mpya kutoka Burkina Faso Stephan Aziz Ki akiwa na Denis Nkane.

Winga hatari Dickson Ambundo akiwa na beki  David Bryson, wakijifua na mazoezi

PICHA NA MTANDAO WA YANGA

…………………………

WACHEZAJI wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara Timu ya Yanga wameendelea kujifua vikali katika viwanja vya Avic Town Kigamboni jijini Dar es salaam.

Yanga wameweka kambia kwa ajili ya Pre-season ya kujiandaa na Michuano mbalimbali ikiwemo wiki ya Mwananchi Agosti 6,2022,Ngao ya Jamii Agosti 13,2022 dhidi ya Watani zao Simba,Ligi Kuu Agosti 17 pamoja na Michuano ya Klabu Bingwa Barani Africa.

About the author

mzalendoeditor