Burudani Featured

DK.MNATA ATOA WITO KWA WAWEKEZAJI KUJITOKEZA KUFADHILI SHUGHULI ZA UTAMADUNI

Written by mzalendoeditor
Na Shamimu Nyaki -WUSM
Mkurugenzi Msaidizi Lugha, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Resan Mnata, ametoa wito kwa Wadau wa Utamaduni kujitokeza kufadhili na kuunga mkono shughuli za Utamaduni nchini.
Dkt. Mnata ametoa rai hiyo Julai 23, 2022 Chamwino Dodoma,  wakati wa Tamasha la 
13 la Muziki wa Cigogo  katika Kijiji Cha Chamwino Ikulu.
Aidha Dkt. Mnata ametoa pongezi kwa Dkt. Kedmon  Mapana, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambaye ndiye mwanzilishi wa  Tamasha hilo ambalo limesaidia kueneza na kukuza Mila na Desturi za Wagogo.
 Pia Dkt. Mnata  ameitaka  Mikoa mingine kufanya matamasha kama hayo katika kukuza na kuendeleza mila,tamaduni na desturi  ili kujenga Umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
Vilevile Dkt. Mnata ametoa wito kwa  jamii kujitokeza kwa wingi Agosti 23, 2022 kuhesabiwa.
Tamasha la Cigogo linqfanyika kwa siku tatu  Julai 22 hadi 24,2022 likiongozwa na Kauli Mbiu “Elimu ya Sanaa ni Muhimu kwa Maendeleo Endelevu ” linapambwa na ngoma mbalimbali za kitamaduni kutoka kabila la Wagogo Dodoma.
Watumishi wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, wenyeji wa Dodoma na wageni kutoka nje  wameshiriki katika Tamasha hilo.

About the author

mzalendoeditor