Featured Kitaifa

RAIS DKT.MWINYI AGAWA VIFAA MBALIMBALI KWA WANANCHI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akizungumza na  Wananchi katika Uwanja wa Mpira wa Paje,mara baada ya kugawa  vifaa mbali mbali  vya Uvuvi,Mwani pamoja na Zawadi mbali mbali  ambapo  anakamilisha kutimiza Ahadi zake alizozitoa pamoja na   kukagua miradi ya maendeleo akiwa katika ziara ya Wilaya ya Kusini Unguja .[Picha na Ikulu] 22/07/2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wapili kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusinmi Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid (mwenye kipaza sauti) leo katika uwanja wa mpira Paje Wilaya ya Kusini ili kukabidhi Boti za Uvuvi,zana za Mwani na Bajaji kwa watu Wenye mahitaji  maalum akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilaya ya Kusini Unguja.[Picha na Ikulu] 22/07/2022. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akimkabidhi Boti ya Uvuvi Nd,Uhuru Suleiman wa kijiji cha Paje  katika uwanja wa mpira  Wilaya ya Kusini  akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilaya ya Kusini Unguja na Kukabidhi vifaa kwa Wananchi.[Picha na Ikulu] 22/07/2022. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akisikiliza maelezo yaliyotolewa kabla kukabidhi Bajaji kwa Watu wenye mahitaji maalum  katika uwanja wa mpira Paje Wilaya ya Kusini leo  katika hafla ya ugawaji wa vifaa mbali mbali vya Uvuvi akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilaya ya Kusini Unguja leo.[Picha na Ikulu] 22/07/2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akimkabidhi Mfano wa Hundi ya Shilingi Millioni 65 Mwenyekiti wa Kikundi Mtule Amcos Nd,Mgana Zidi Khamis(wa pili kulia) katika hafla ya ugawaji wa vifaa mbali mbali kwa wananchi katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilaya ya Kusini Unguja leo(kulia) Meneja Mtule Amcos Bi.Latii Adalla Adalla .[Picha na Ikulu] 22/07/2022.

Wanannchi wa Kijiji cha Paje wakiwa katika  hafla ya ugawaji wa vifaa mbali mbali  vya Uvuvi,Mwani pamoja na Zawadi mbali mbali vilivyotolewa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akikwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilaya ya Kusini Unguja .[Picha na Ikulu

About the author

mzalendoeditor