Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali
Mwinyi akikabidhi boti sita za uvuvi na vifaa vyake kwa kikundi cha wavuvi
katika Shehia ya Jongoe Kisiwa cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa
Kaskazini Unguja, Zanzibar leo Julai 20, 2022 kupitia Mradi wa Kuhimili
Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR)
unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Chilo akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya boti sita
za uvuvi na vifaa vyake iliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Shehia ya Jongoe Kisiwa
cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Chilo akishiriki matukio mbalimbali wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye
alikabidhi boti sita za uvuvi kwa vikundi vya vya Shehia ya Jongoe Kisiwa cha
Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar leo Julai 20,
2022 kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo
Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Chilo akiwa katika boti kutokea Bandari ya Mkokotoni kuelekea Kisiwa cha
Tumbatu kushiriki hafla ya makabidhiano ya boti sita za uvuvi kwa kikundi cha
Shehia ya Jongoe leo Julai 20 kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi
kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu
wa Rais.
Sehemu ya boti za uvuvi zilizokabidhiwa kwa kikundi cha uvuvi cha Shehia ya Jongoe leo Julai 20 kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi
kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
…………………………………
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis
Hamza Chilo ametoa rai kwa wanufaika wa mradi wa boti za uvuvi
zilizotolewa kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia
Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) kutofanya shughuli za kibinadamu zinazochangia
uharibifu wa mazingira.
Ametoa rai hiyo leo Julai 20, 2022 wakati wa hafla ya makabidhiano ya boti sita
za uvuvi zilizokabidhiwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika Shehia ya Jongoe Kisiwa cha Tumbatu Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.
Mhe. Chilo alisema boti hizo zitumike kuleta tija katika mapambano ya
athari za mabadiliko ya tabianchi zinazoikabili nchi yetu na duniani kwa ujumla, hivyo ni wajibu wa wanufaika wa mradi huo kuhakikisha wanatunza vyanzo vya maji, kufanya kilimo endelevu.
Alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inaendeleza ushirikiano mzuri uliopo
baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na ndiyo maana inatekeleza miradi hii.
”Leo zinakabidhiwa boti hizi kwa vikundi vya wavuvi ambao ndio wanufaika
wakuu kwa hiyo nitoe rai kwenu mtunze vyanzo vya maji ili viumbe vilivyomo
navyo viweze kuishi na kutunzwa kwakuwa mazingira ndio kila kitu kwa vizazi vya sasa bna
vijavyo,” alisema Chilo.
Aidha, Mradi wa EBARR ni wa kipindi cha miaka mitano ambapo utekelezaji wake ulianza mwaka 2018 na utakamilika mwaka huu 2022 na unatekelezwa katika Wilaya za Mvomero (Morogoro), Simanjiro (Manyara), Kishapu (Shinyanga), Mpwapwa (Dodoma) Tanzania Bara na Kaskazini A – Unguja, upande wa Zanzibar.
Maeneo ya Mradi yalichaguliwa kwa kuzingatia maeneo yenye ukame yenye jamii za wakulima, wafugaji, na wavuvi kwa lengo la kuongeza uwezo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika jamii za vijijini kwa kuimarisha mifumo ikolojia na shughuli mbadala za kujiongezea kipato.