Baada ya Uzinduzi wa Kola online TV kupitia mtandao 15 July 2022,sasa ni Kola Liquid Soap leo 20 July 2022,ni sabuni inayosafisha sakafu,maliwato, kufua, kuoshea vyombo, kunawa na kadhalika.
Mkurugenzi wa Kola Products ikiwemo Kola Liquid Soap na Kola online TV bi. Josephine Charles ameshauri wananchi kutumia bidhaa hiyo inayotengenezwa Shinyanga bila uchakachuzi wowote.
“Imekuwa kama utamaduni watengezaji wa bidhaa hii ya sabuni kuchakachua kwa kupunguza vipimo vya malighafi pamoja na kujaza maji jambo ambalo linamfukuza mteja akinunua mara moja harudi, lakini Kola Liquid Soap ipo tofauti na zingine na tunauza kwa bei ya kawaida kabisa na mteja lazima arudi kutokana na ubora atakaoukuta” , amesema bi. Josephine.
“Nimeamua kuzindua mwezi wa Saba kwa kuwa ni mwezi niliozaliwa mimi,kwa hiyo ni kiashiria tosha kuwa nimekua na nina uwezo wa kumiliki vitu vyangu mwenyewe na kuviendeleza”, ameongeza.
Amesema Kola pia litakuwa ni darasa kwa watakaopenda kujifunza kutengeneza sabuni hiyo “Hatutaishia kuuza tu bali pia tutakuwa tunafundisha namna ya kutengeneza sabuni kupitia Kola Online TV ili kuongezea watu maarifa na kuwafanya waweze kujitegemea”.
Amefafanua zaidi kuwa kupitia Kola Products wana bidhaa nyingi ikiwemo Kola Flour (unga wa Lishe, Sembe na Dona) na bidhaa zingine ambazo wataendelea kuzindua kila uchwao.
“Kola Liquid Soap tunasema Usafi ni Afya”, weka oda yako mapema utengenezewe sabuni ya uhakika piga simu namba 0784129646 au bonyeza link hii ili uweze kujifunza namna ya kutengeneza bidhaa hiyo https://youtube.com/channel/UCHlPIovw52Ai7k8iba9UJbg