Featured Kitaifa

HOSPITALI YA JIJI TANGA YAIPONGEZA SERIKALI KUWASOGEZEA VIFAA TIBA

Written by mzalendoeditor

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tanga Jiji (DMO) Dkt. Charles Mkombe akizungumza na maafisa kutoka Bohari ya Dawa (MSD) na waandishi wa habari leo Julai 18,2022 mkoani Tanga.Mashine ya ultrasound ambayo imekabidhiwa katika Hospitali ya Wilaya Tanga Jiji ambayo ni ya kisasa kwa ajili ya kutoa huduma katika hospitali hiyo Mteknolojia wa Mionzi wa Hospitali ya Wilaya Tanga Jiji Dkt.Mohamed Ally akionesha mashine mpya ya ultrasound waliyoipokea hivi karibuni, kwa ajili ya kuongeza nguvu za kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya katika hospitali hiyo ambayo ina miaka miwili tangu ifunguliwe Baadhi ya Vifaa tiba kwa ajili ya upasuaji vikiwa vimehifadhiwa kwenye chumba maalumu hospitali ya Wilaya Tanga jiji. Hospitali hii ni miongoni mwa vituo vipya 67 vilivyojengwa na kukarabatiwa na serikali.

***********************

NA MWANDISHI WETU

HOSPITALI ya jiji la Tanga inatarajia kuanza upasuaji wa uzazi pingamizi na kupokea wagonjwa wa rufaa ifikapo Septemba mwaka huu, baada ya kupokea vifaa tiba vya kisasa kutoka Bohari ya Dawa (MSD).

Akizingumza leo Julai 18,2022 Mkoani humo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tanga Jiji (DMO) Dkt. Charles Mkombe, amesema hospitali hiyo ya Jiji ni kati ya vituo vya kutolea huduma za afya 67 vipya na vilivyofanyiwa ukarabati na serikali.

“Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imelenga kuziwezesha hospitali hizo kupokea wagonjwa wa rufaa na tayari tumepokea vifaa tiba vya kisasa vilivyotolewa na serikali kutoka MSD ambapo hivi karibuni tutaanza upasuaji,”amesema.

Dkt.Charles, ameeleza kuwa lengo la maboresho hayo katika sekta ya afya hususani  huduma ya mama na mtoto ni kuimarisha sekta hiyo na kuchochea uchumi.

Ameongeza kuwa, hospitali hiyo inayohudumia wananchi 260,000 ilikuwa haifanyi upasuaji na kwa maelekezo ya Rais Samia Suluhu maandalizi yote yamekamilika ikiwemo watumishi wa kutosha, mazingira wezeshi yenye majengo 10 ya kisasa na vifaa tiba vya kisasa.

Naye Mteknolojia wa Mionzi wa hospitali hiyo Dkt.Mohamed Ally, amesema vifaa tiba na mashine zilizopokelewa kutoka MSD ni pamoja na vifaa vyote vya wodi ya kujifungua ikiwemo mashine ya ultrasound yenye uwezo wa kupima moyo na kuchapa picha.

Aidha inaweza kupima afya ya mtoto iwapo amezaliwa salama bila tatizo, mfumo wa damu wa mama, matarajio ya kujifungua, mtoto amefikisha muda gani akiwa tumboni na namna alivyokaa kabla ya kujifungua.

Pia ina mfumo wa mawasiliano kwa kutuma taarifa za mgonjwa moja kwa moja kwa daktari bila ulazima wa kuchapa picha kwenye karatasi.

“Kwetu sisi watoa huduma tukiwa na vifaa kama hivi na mazingira wezeshi tunaona raha hata kufanya kazi, tunamshukuru sana Rais Samia na serikali yake kwa maboresho ya huduma za dharula mama na mtoto,”amesema.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt.Rashid Said, amesema hospitali ipo nje ya jiji la Tanga, ambapo inawasaidia wananchi wa pembezoni kutofuata huduma hizo mjini.

Amesema hatua ya kukamilika kwa utoaji huduma ikiwemo chumba cha upasuaji na  wodi ya wagonjwa mahututi itawezesha ipasavyo utekelezaji wa sera za sekta ya ipasavyo.

About the author

mzalendoeditor