Featured Kitaifa

SERIKALI  YAJIPANGA KUENDELEZA MIRADI MBALIMBALI KATIKA SEKTA YA MADINI HAPA NCHINI

Written by mzalendoeditor

Na. Costantine James, Geita.

Waziri wa Madini Mhe, Dkt. Doto Biteko amesema serikali imejipanga kuhakikisha inashirikiana vizuri na wawekezaji mbalimbali katika sekita ya madini hapa nchini kwa lengo la kukuza uchumi wa taifa.

Amesema hayo leo mkoani Geita wakati alipotembelea mgodi wa Buckreef uliopo kata ya Lwamugasa wilaya ya Geita Mkoani Geita na kujionea jinsi mgodi huo unavyofanya kazi.

Dkt. Biteko amesema serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassani imejipanga kikamilifu miradi yote iliyopo kwenye sekta ya madini lazima iendelezwe kwa lengo la kukuza uchumi wa taifa na wananchi kwa ujumla.

“Matarajio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kwamba miradi yote ambayo ipo kwenye Sekta ya Madini iweze kuendelezwa,”amema Dkt. Doto Biteko waziri wa Madini.

Dkt. Doto Bitekoameupongeza pia mgodi wa Buckreef kwa kutoa ajira kwa Watanzania wanaofanya kazi mbalimbali za uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huo.

Amesema, mgodi wa Buckreef umetoa ajira za moja kwa moja 354 kwa Watanzania katika nafasi mbalimbali katika mgodi huo.

Amewataka wafanyakazi waliopewa ajira katika mgodi huo kuhakikisha wanajenga taswira nzuri kwa kuwa wazalendo na waaminifu katika kazi zao Kwani kupitia uaminifu wawekezaji watatoa fursa zaidi kwa Watanzania kuweza kufanya kazi mbalimbali katika migodi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Rosemary Senyamule ameupongeza mgodi wa Buckreef kwa kusimamia kikamilifu swala usalama kwa wafanyakazi katika Mgodi huo.

Senyamule amemuomba waziri wa madini Dkt. Doto Biteko kuleta wawekezaji wengi zaidi mkoani Geita kutokana na mkoa huo kuwa na maeneo mengi ya kuwekeza hasa katika miradi ya Madini.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buckreef Mhandisi Gaston Mujwahuzi amesema Mgodi huo kwa sasa unauwezo wa kuzalisha tani laki moja kwa mwezi.

Mhandisi Mujwahuzi amesema wataendelea kuwashirikisha wananchi katika huduma za kijamii kwa ajili ya manufaa ya watu wote.

Kampuni ya Dhahabu ya Buckreef ikishirikiana na mbia mwenza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) inajushughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu hata hivyo Kampuni ya Buckreef inamiliki hisa kwa asilimia 55 na STAMICO inamiliki hisa asilimia 45.

About the author

mzalendoeditor