Featured Kitaifa

GILITU : VIJANA MSING’ANG’ANIE TU KUKAA MJINI, WEKEZENI KWENYE KILIMO

Written by mzalendoeditor
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akionesha jinsi mafuta ya alizeti yanavyozalishwa katika kiwanda chake kilichopo Mjini Shinyanga
Muonekano wa mtambo wa Solvent wa kukamua mafuta ya pamba uliopo kwenye Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga
Muonekano wa mafuta ya kupikia ya alizeti yanayozalishwa katika Kiwanda cha Gilitu Enterprises Ltd Mjini Shinyanga
Muonekano wa mafuta ya kupikia ya alizeti na pamba yanayozalishwa katika Kiwanda cha Gilitu Enterprises Ltd Mjini Shinyanga
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula amewataka vijana kujishughulisha na kuachana na tabia ya kukaa tu mjini bali wawekeze katika Kilimo kutokana na kwamba kilimo ni biashara na Serikali imetoa kipaumbele kwa sekta ya kilimo ili kumkomboa mwananchi kiuchumi.
 
Makula ametoa rai hiyo Julai 15,2022 wakati wa ziara ya Maafisa Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo na Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kutembelea wadau wa Pamba kwenye baadhi ya mikoa inayolima zao la Pamba Kanda ya Ziwa ambapo wamejionea uwekezaji mkubwa wa Mwekezaji huyo mzawa ambaye anasindika mafuta ya alizeti na pamba, kuuza mashudu nje ya nchi na kutengeneza sabuni zitokanazo mazao hayo.
 
Makula amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekipa kipaumbele kilimo na imekuwa bega kwa bega na wakulima kwa kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo za kilimo ambapo hivi karibuni umezinduliwa mfumo wa utoaji wa ruzuku ya mbolea kwa wakulima na maafisa ugani wamepewa vitendea kazi ili kuhakikisha kuwa Kilimo kinatoa ajira kwa vijana na kuleta maendeleo katika nchi.
 
“Vijana msing’ang’anie tu kukaa mjini, wekezeni kwenye kilimo njia ni nyeupe serikali imetupa nguvu katika kilimo. Naomba turudi kijijini tukalime, twendeni tukaanzishe hata kilimo cha umwagiliaji kwani kilimo ni biashara na kinalipa”,amesema Makula.
 
“Vijana msiwe waoga wa kuthubutu, jaribuni kufanya kila kitu badala ya kulia lia kuwa hakuna ajira. Ingia kwenye kilimo, wenye mitaji wekezeni kwenye kilimo kwani Mhe. Rais Samia yuko bega kwa bega na wakulima na tunaye Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe anatusikiliza na na kutusaidia sana. Tunakoelekea ni kuzuri na sisi tuliowekeza tumejifunza mengi na tupo tayari kuwasaidia wengine”,ameongeza Makula.
 
Makula ambaye alianza ujasiriamali mwaka 1997 kwa kuuza mafuta kwenye chupa ‘vibaba’ na sasa ni mwekezaji mkubwa amesema ili nchi ipate maendeleo ni lazima kuwe na viwanda lakini viwanda hivyo viwe na malighafi ili kuwa na uzalishaji endelevu wa bidhaa.
 
“Ili nchi yetu ipate uchumi tunahitaji viwanda viwe vingi hivyo vijana wanapaswa kuchangamkia fursa katika kilimo ili viwanda hivi vilivyopo vipate mali ghafi. Mfano hapa nina kiwanda lakini malighafi hazitoshi kufanya uzalishaji wa mafuta ya pamba na alizeti. Kiwanda changu kina uwezo mkubwa wa kusindika mafuta kwa siku lakini kwa sasa uzalishaji wetu ni asilimia 30 hadi 40 kwa siku kutokana na kukosa malighafi. Wananchi wakilima kwa tija tutapata malighafi nyingi”,amesema.
 
Aidha amewataka wananchi wakiwemo vijana kulima zao la pamba na alizeti kwa tija ili kupata mazao mengi hali itakayosaidia kukabiliana na changamoto ya uhaba wa mafuta nchini akibainisha kuwa viwanda vya kusindika mafuta vipo tatizo ni upatikanaji wa mali ghafi kwa ajili ya kuendesha viwanda vilivyopo,hivyo malighafi zikipatikana za kutosha uhaba wa mafuta utakiwa historia.
 
Makula ametumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuacha kuchanganya biashara na starehe na tamaa ya kutaka kufanikiwa kwa njia za mkato bali wawe na wivu wa mafanikio huku akiwataka kumtanguliza Mungu katika shughuli zao.
 
“Ukianza uwekezaji achana na starehe kwa sababu starehe na biashara haviendani. Vijana mstake kufanikiwa kwa njia ya mkato ‘kuanza juu’ kwani mfanyabiashara aliyefanikiwa alianzia chini na kuwa na uchungu na kile ulichonacho. Mimi nilianza na mtaji wa shilingi 15,000/= lakini sasa nina mtaji wa takribani shilingi Bilioni 25”,amesema.
 
“Biashara ni wewe mwenyewe hivyo ni lazima uisimamie mwenyewe, acha u bosi lakini pia tafuta watu wenye akili ya kukusaidia kazi na jitahidi walau kujiendeleza kielimu na ukumbuke kuwa na nidhamu ya fedha , kujituma kuwa mvumilifu, mwaminifu na mwadilifu kwani kuna dhoruba nyingi kwenye utafutaji hivyo usikate tamaa, hizo changamoto zitumie kama fursa”,ameeleza Makula.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula mafuta ya alizeti yanavyozalishwa katika kiwanda chake kilichopo Mjini Shinyanga
Sehemu ya kuingia kwenye mtambo wa Solvent wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akionesha sehemu ya mtambo wa Solvent unaokamua mafuta ya pamba katika kiwanda chake cha mafuta ya pamba na alizeti ‘SANICO’ kilichopo Mjini Shinyanga

Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akionesha sehemu ya mitambo ya kukamua mafuta ya pamba na alizeti katika kiwanda chake cha mafuta ya pamba na alizeti ‘SANICO’ kilichopo Mjini Shinyanga

Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akionesha sabuni itokanayo na zao la alizeti na pamba katika kiwanda chake cha mafuta ya pamba na alizeti ‘SANICO’ kilichopo Mjini Shinyanga
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula akionesha nembo ya mafuta ya pamba na alizeti ‘SANICO’  yanayotengenezwa katika kiwanda chake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usindikaji Mafuta ya Gilitu Enterprises Ltd ya Mjini Shinyanga, Gilitu Makula  (kulia) na Meneja wa Kiwanda cha Gilitu Enterprises Ltd , Freedom Maro na Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo, Bi. Nyabaganga Talaba (katikati) wakionesha mafuta ya  alizeti ‘SANICO’. Kiwanda hicho pia kinazalisha mafuta ya pamba, sabuni na mashudu.
 
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
About the author

mzalendoeditor