Featured Kitaifa

PICHA: SPIKA DKT. TULIA ATETA NA BALOZI POLEPOLE JIJINI LILONGWE

Written by mzalendoeditor

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi Jijini Lilongwe.

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole (kushoto) alipomtembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe. Wengine ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioambatana na Mhe. Spika.

Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole akiwasilisha taarifa ya Mahusiano baina ya Tanzania na Malawi mbele ya Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) katika ofisi za Ubalozi huo Jijini Lilongwe nchini Malawi. Wengine ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioambatana na Mhe. Spika

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipokea taarifa ya Mahusiano baina ya Tanzania na Malawi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole alipomtembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole alipotembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole (kulia kwake) alipotembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe nchini Malawi. Kuanzia kushoto ni Wabunge wa Bunge la Tanzania walioambatana na Mhe. Spika ambao ni Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Kassim Haji, Mhe. Shally Raymond na Mhe. Dkt. Alfred Kimea.

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongozana na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ubalozini hapo Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ubalozini hapo Jijini Lilongwe nchini Malawi.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

About the author

mzalendoeditor