WATU 15 wameuawa kwa kupigwa risasi huku wengine 11 wakijeruhiwa baada ya kuvamiwa na majambazi katika baa moja iliyopo kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo ya habari nchini humo, tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Jumapili, Julai 10, muda mfupi baada ya saa sita usiku.
Watu wengine 11 walijeruhiwa katika kisa hicho ambapo walikimbizwa hospitali huku nane kati yao wakiwa mahututi.