Featured Kitaifa

WAZIRI MCHENGERWA AMWAKILISHA RAIS SAMIA MSIBA WA BI.HINDU

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na
Michezo. Mhe,  Mohamed Mchengerwa wa pili kutoka kushoto akiwa msibani na waombolezaji wengine
Na John Mapepele
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia  Suluhu Hassan leo Julai
10, 2022 ametoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa  msanii  mkongwe
wa Filamu nchini Chuma Seleman maarufu kama Bi. Hindu.
Salamu
hizo zimetolewa kwa niaba yake na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na
Michezo. Mhe,  Mohamed Mchengerwa Magomeni jijini Dar es Salaam 
nyumbani kwa marehemu kabla ya kwenda kupumzishwa kwenye nyumba yake ya
milele.
Akimzungumzia
marehemu, Mhe. Mchengerwa amesema, Mhe. Rais amemwelezea   Bi. Hindu
kuwa ni msanii aliyetoa mchango mkubwa katika tasnia ya Sanaa hapa
nchini.
“Bi Hindu ametoa 
elimu ya sanaa kwa wasanii wengi sana, Serikali inatambua mchango wake.
Mhe Rais amepokea msiba huu kwa msiba huu kwa mshituko mkubwa”.
Amefafanua Mhe, Mchengerwa
Aidha, amesema marehemu Hindu amefariki wakati Serikali inafanya mapinduzi makubwa  katika sekta za Sanaa.
Katika msiba huo Katibu Mwenezi wa CCM komrade Shaka na viongozi mbalimbali wa Serikali, Michezo na Sanaa wamehudhuria.

About the author

mzalendoeditor