Featured Kitaifa

MBUNGE LOWASSA: MSAADA WA MATIBABU YA MACHO ILIYOTOLEWA WILAYANI HUMO NA AL ATA’A CHARITABLE FOUNDATION IMEPUNGUZA CHANGAMOTO ILIYOKUWEPO.

Written by mzalendoeditor
Mtaalamu wa macho kutoka hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha Maunt Meru akimwekea dawa ya macho mmoja wa wananchi wilayani Monduli.
Mtaalamu wa macho akiwafanyia wananchi vipimo vya awali vya macho wilayani Monduli.
Baadhi ya wananchi kutoka katika kata mbalimbali za wilaya ya Monduli waliojitokeza kupata huduma ya macho katika hosipitali ya wilaya ya Monduli kwa ufadhili wa shirika la Al Ata’a Charitable foundation.
Mkurugenzi Mtendaji wa Al Ata’a Cheritable Foundation Ahmed Elhamrawy  akiongea wakati wa uzinduzi wa utoaji wa huduma za macho Wilaya ya Monduli kwa ufadhili wa shirika hil
 Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredy Lowasa akizindua zoezi la utoaji wa huduma ya macho katika hosipitali ya wilaya ya Monduli kwa ufadhili wa shirika la Al Ata’a Charitable foundation.
Mratibu wa macho Mkoa wa Arusha Dkt Lawrence Mremi akiongea na waandishi wa habari katika utoaji wa huduma ya macho wilayani Monduli 
……………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha  Fredy Lowassa amesema kuwa kitendo cha wafadhili kutoka shirika la Al Ata’a Charitable foundation kwenda kupima macho kwa jamii ya wafugaji waishio pembezoni imesaidia  kupunguza changamoto ya ukosefu wa matibabu  kutokana na uhitaji mkubwa uliopo
Fredy  ameyasema hayo wakati akizindua zoezi hilo kwa wilaya ya Monduli ambapo alisema kuwa kwa siku moja tuu wamehufumiwa watu zaidi ya 100 na kuwafanyia upasuaji wa mtoto wa jicho watu zaidi ya 10 kwa siku hizi tatu wataweza kuwatibia wengi zaidi ambapo alisema Hilo sio jambo dogo bali ni jambo la kushukuru sana.
Alisema kuwa Jimbo lake ni wilaya za pembezoni ambapo Kuna huduma ambazo serikali inajitahidi lakini Kuna huduma hawataweza kuzipata bila kupata wadau au washirika kama hao na hayo yote yamewezekana baada ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu kuingia madarakani kwani ameweza kuifua nchi katika sekata mbalimbali.
 “Mafanikio hayo yote ya kuja kwa wafadhili hawa yamechangiwa na  juhudi za Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ya kufungua Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo kupitia filamu ya Royal Tour ambayo imechangia maswala mengi kufunguka,”Alisema Fredy Lowasa
“Tunawashukuru sana wafadhili wetu kwa kuja kutoa huduma hii ya macho bure  kwa siku tatu  na kutoa  miwani  sambamba na kuwafanyia upasuaji ambao mnawaona wana shida kubwa   jambo ambalo linawasaidia Sana wananchi wetu hasa hawa waishio pembezoni  kwani wamekuwa wakisahaulika sana.”Alisema.
Alieleza kuwa kutokana na juhudi za Rais wafadhili hao Wana amani ndio maana wameenda hadi Monduli lakini pia wanasaidia na maeneo mengine sio kwenye suala la macho tuu pia wanajenga visima, madarasa, misikiti na kusaidia kutibia magonjwa mengine kama vile kisukari, moyo, magonjwa ya njia ya hewa na mengineyo.
“Wakati mwingine tunajisikia kama wamasai tuko pembeni kidogo kwahiyo tulipata ugeni mkubwa kama huu ambao sio ugeni wa kitalii tuu bali ni ugeni wa kuja kutoa huduma Tena huduma muhimu kabisa ya Afya na wamekuja kwenye jambo ambalo ni nyeti suala la macho ambalo linahitaji utaalamu mkubwa sana, kwakweli lazima tuwashukuru hawa watu,” Alieleza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Al Ata’a Cheritable Foundation, Ahmed Elhamrawy alisema kuwa anamshukuru Rais wa Tanzania kwa kuwa anazingati sana sekta ya afya ambapo wao wanafanya kazi nyingi lakini zaidi ni katika sekta hiyo na huduma wanayoitoa kwa jamii mbalimbali ni endelevu  na wanatoa huduma hizo kwa kudhaminiwa na Qatar Charity ambayo ni taasisi kubwa inayofanya mambo ya heri.
Amesema kuwa, kwa  upande wa macho wanakuwa na kambi kwa ajili ya macho, ambapo kwa kila Kambi wanalenga kufikia wananchi 1,000 huku katika hao wakilenga kufanyia upasuaji wananchi 200 kwa kila Kambi ,ambapo amesema mwitikio  bado ni mdogo kulingana na matarajio waliyoweka,huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo.
Alifafanua kuwa wanawafikia watu kulingana na utaratibu wanaopewa na wizara ya Afya juu ya tatizo husika, kwani tatizo la macho ni tatizo kubwa na hasa linahitaji mtu apate matibabu katika hatua za mwanzoni na mtu akichelewa tatizo linazidi kuwa kubwa.
Naye Mratibu wa macho Mkoa wa Arusha Dkt Lawrence Mremi alisema kuwa,  wameweza kuwafikia watu zaidi ya 800 Longido na kufanya oparesheni zaidi ya 50 ambapo katika wilaya ya Monduli wanatarajia pia idadi itaongezeka kwani nafasi ni nyingi za watu kupata huduma hiyo ambapo pia wameweza kuwafuata na kuwaleta kupata huduma watu kutoka Mto wa Mmbu.
Alisema kuwa ni vema watu wakachangamkia huduma hiyo iliyoletwa na wafadhili hao kwani kuna changamoto ya   uhaba wa wataalamu wa macho ambapo kwa halmashauri ya wilaya ya Monduli wapo wataalamu watatu tu katika kitengo cha macho jambo ambalo ni changamoto kubwa hasa katika utoaji wa elimu kutokana na kutokidhi mahitaji  kulingana na idadi ya wananchi wenye uhitaji.
Aidha wananchi waliojitokeza kupata huduma hiyo  Mery Mrina kutoka  Monduli  alisema kuwa anawashukuru sana wafadhili hao kwa kuwaletea  huduma hiyo hadi nyumbani kwani ameweza kupimwa macho na kupewa miwani bure,huku akiwataka kuwatembelea  mara kwa mara  na kwenda maeneo ya vijijini kulipo na wahitaji wengi zaidi na hawana sehemu ya kupata huduma hiyo.
Leokadia Macha ambaye pia ni mkazi wa Monduli Alieleza kuwa amepata huduma nzuri kwa muda mfupi ambapo ametibiwa lakini pia kupewa elimu na ushauri wa namna ya kuendelea kuyatunza macho yake ili kuepuka kuendelea kupata madhara mengine bure bila malipo yoyote
Hatahiyo tasisi hiyo mpaka Sasa imeshafanya kambi za afya katika mikoa ya Kigoma, Dar es salaam, Pwani, Dodoma na Arusha ambapo wanatarajia kwenda mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya suala zima la afya kwa ujumla.

About the author

mzalendoeditor