Featured Kitaifa

IGP SIRRO HALI YA NCHI YETU NI SHWARI

Written by mzalendoeditor

 

Matukio mbalimbali pichani yakimuonesha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, wakati alipotembelea maonesho ya 46 ya Kimataifa ya biashara ambayo bado yanaendelea jijini Dar es salaam. IGP Sirro aliwataka wananchi kuendelea kutembelea maonesho hayo ambayo kwasasa yamekuwa na vitu vingi vizuri ikiwemo elimu inayotolewa na Jeshi la Polisi kuhusu namna ya kutambua uhalifu na kukabiliana matukio ya uhalifu na wahalifu. Picha na Jeshi la Polisi

***********************

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema hali ya usalama nchini imeendelea kuwa shwari kwani hadi sasa hakuna matukio makubwa ya uhalifu na wahalifu yaliyoripotiwa na kwamba amewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali kuendelea na mikakati yao ya uwekezaji kwa lengo la kuleta maendeleo.

IGP Sirro amesema hayo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea maonesho ya 46 ya kimataifa ya biashara maarufu Saba saba na kutoa angalizo kwa watu wenye nia ovu ya kutaka kuvuruga amani na kwamba Jeshi la Polisi alitosita kuwachukulia hatua za kisheria.

About the author

mzalendoeditor