RAIS wa Klabu ya Yanga,Mhandisi Hersi Said amemtambulisha mchezaji wa Newcastle United ya Uingereza,Gael Bigirimana katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere unapofanyika uchaguzi wa timu hiyo.
Akizungumza wakati akimtambulisha mchezaji huyo mbele ya wajumbe Rais wa Yanga amesema kuwa wao wanasajili wachezaji wakubwa na saa tisa usiku watamtambulisha mchezaji mwingine na kuhitimisha Siku ya Jumatatu kumtangaza mchezaji mpya na kufikia idadi ya wachezaji watano waliosajiliwa.
Mpaka sasa Bigirimana anaungana na Bernard Morrison ‘BM3’ kutoka nchini Ghana pamoja na Mshambuliaji Lazarous Kambole kutoka Zambia.Pia mchezaji amepita katika vilabu vya Coventry City, Newcastle United, Rangers na klabu ya Grentoran football club yenye maskani yake huko Ireland kaskazini
Aidha mwaka 2013 aliwahi kuichezea timu ya taifa ya ya vijana U20 ya England, alicheza mechi mbili.