Featured Kitaifa

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAIPONGEZA TAWA

Written by mzalendoeditor

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo,akisalimiana na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka mara baada ya kufanya ziara ya  kukagua miradi ya maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambana dhidi ya Uviko-19 katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara kwa ajili ya  kukagua miradi ya maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambana dhidi ya Uviko-19.

Afisa Uhifadhi Miundombinu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Noti Mgaya akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa miradi ya Miundombinu chini ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ikikagua mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 47.2 katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

Afisa Uhifadhi Miundombinu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Noti Mgaya akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu ujenzi wa Picnic Site katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

Kamishna Msaidizi Khadija Malongo,akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu ujenzi wa Barabara katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ,akitoa ufafanuzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 47.2 katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

WANYAMA Tembo na Twiga wakiwa katika Pori la Akiba la Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kukagua miradi ya maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambana dhidi ya Uviko-19 katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja,akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ya kukagua miradi ya maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambana dhidi ya Uviko-19 katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dk.hamis Mkanachi,akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ya kukagua miradi ya maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambana dhidi ya Uviko-19 katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

KAIMU Naibu Kamishna wa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),Mlage Kabange,akitoa wasilisho la taarifa ya utekelezaji wa miradi ya UVIKO-19 katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Eliamani Sedoyeka akiishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti baada ya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi wa lango la kuingilia wageni, barabara ya kilomita 47.2 na ujenzi wa Picnic Site. kwenye Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara ya Kamati ya kukagua miradi ya maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambana dhidi ya Uviko-19 katika Pori la Akiba Mkungunero  lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. .

………………………

Na Alex Sonna-KONDOA

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Bajeti imepongeza na kuridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Miundombinu inayotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) katika Pori la Akiba Mkungunero lililopo katika mikoa ya Dodoma na Manyara. 

Akizungumza katika ziara ,Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Daniel Sillo,amesema kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa lango la kuingilia wageni, barabara ya kilomita 47.2 na ujenzi wa Picnic Site. kwenye Pori la Akiba Mkungunero iliyogharimu kiasi cha shilingi Milioni 672.

Miradi hiyo imejengwa kwa kupitia fedha za Mradi wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Mhe.Sillo  amempongeza  Spika wa bunge  kwa kuridhia Kamati ya Bajeti kupitisha shilingi trilioni 1.3 ambapo kati ya hizo Wizara ya Maliasili na Utalii ilipewa shilingi bilioni 90.2.

Amesema  Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania  (TAWA) ilipewa shilingi bilioni 12.9 huku Pori la Akiba la Mkungunero likipatiwa shilingi milioni 672.

“Nichukue nafasi hii kuipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa usimamizi mzuri wa miradi hii na muendelee na hatua hii kwani inafungua fursa na Rais Samia ameonesha njia kupitia Royal Tour ukienda Arusha Hoteli zimejaa ‘amesema Mhe.Sillo

Amesema sekta ya utalii inachangia asilimia 17 ya pato la Taifa na  asilimia 25 ya  pato la kigeni hivyo anaamini kwa siku za mbele uchangiaji utaongezeka zaidi.

“Niwashauri endeleeni kusimamia miradi hii niwaombe msimamie vizuri miradi hii ili iweze kuleta  tija,”amesema Mhe.Sillo 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja amesema TAWA  ilitengewa shilingi  bilioni 12.9 ambazo zilipaswa kutetekeleza miradi mbalimbali.

”Pori la Mkungunero ilitengewa shilingi  milioni 672 ambazo zilikuwa zimepangwa  kutekeleza  miradi mitatu ambayo ni ujenzi wa lango la kuingilia  wageni, ujenzi  wa barabara na ujenzi wa Picnick site.”amesema Mhe.Masanja

Awali Kaimu Naibu Kamishna wa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),Mlage Kabange,amesema Pori la Mkungunero ni miongoni mwa mapori  27 yanayosimamiwa na TAWA  ambapo pori hilo lina ukubwa wa kilomita za mraba 743.

Amesema asilimia 92 ya eneo la pori hilo lipo  Dodoma katika Wilaya ya  Kondoa na asilimia  8 ipo katika Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.

Amesema pori hilo lina faida za kiikolojia na ni makazi ya wanyama mbalimbali wakiwemo Tembo na Tandala.

“Hapa kuna Simba,Chui na kuna nyuki na hapa kuna mambo mazuri sana ikiwemo  ya kiikolojia ambayo inasababisha baadhi ya maeneo hasa vijiji vya jirani kuweza  kupata  maji,”amesema .

Amesema kuna fursa za utalii zinazopatikana kupitia pori hilo  na watu mbalimbali kufika kuwinda na pia  ni dakio la maji katika Mto Tarangire

Amesema TAWA  iliidhinishiwa shilingi  bilioni 12.9 na imepokea fedha zote na tayari imeingia makubaliano na wakandarasi kwa ajili ya kukarabati miradi hiyo.

About the author

mzalendoeditor