Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AFUNGUA JENGO LA HUDUMA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO LA HOSPITALI CCBRT JIJINI DAR ES SALAAM

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wengine wakati akivuta kitambaa kama ishara ya kufungua Rasmi jengo la Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto lililopo kwenye Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi mara baada ya kufungua rasmi jengo la Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto lililopo kwenye Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapongeza na kuwapa zawadi Wanawake waliojifungua katika jengo jipya la Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto lililopo kwenye Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Daktari Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake Issa Rashid kuhusiana na huduma mbalimbali zinazotolewa katika jengo jipya la Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2022.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Bi. Brenda Msangi kuhusiana na huduma mbalimbali zinazotolewa kwenye hospitali hiyo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wauguzi pamoja na madaktari wa Hospitali ya CCBRT waliopo kwenye jengo jipya Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto wakati alipokuwa akikagua huduma mbalimbali katika hospitali hiyo Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Julai, 2022.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wauguzi wanao hudumu katika jengo hilo jipya la huduma ya afya ya mama na mtoto mara baada ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo tarehe 05 Julai, 2022.

About the author

mzalendoeditor