MzalendoBlog
  • Habari
    • Kitaifa
    • Kimataifa
  • Michezo
  • Burudani
  • Makala
Mzalendo
  • Habari
    • Kitaifa
    • Kimataifa
  • Michezo
  • Burudani
  • Makala

Home » RAIS SAMIA ATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU ZOTE ZA KOMBE LA YAMLEYAMLE

Featured • Michezo

RAIS SAMIA ATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU ZOTE ZA KOMBE LA YAMLEYAMLE

3 years ago
by Alex Sonna
52 Views
Written by Alex Sonna

 

Na John Mapepele.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan ametoa
vifaa vya michezo kwa timu zote 45 zinazoshiriki mashindano ya kombe la
Yamleyamle Zanzibar ili timu ziweze kufanya vizuri hatimaye  kuwapata
wachezaji bora na wenye  vipaji ambao wataunganishwa  kwenye timu ya
Taifa.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed
Mchengerwa, Julai 3, 2022 wakati akizindua mashindano hayo yanayofanyika
kwenye Uwanja wa Amani Zanzibar ambapo amesema Mhe. Rais ametoa mipira
45 kwa ajili ya timu hizo na jezi.
“Niwaombe 
tunapojipanga kwenda kuandaa mashindano ya AFCON,  tuleteeni orodha 
ya  vijana wanaofanya vizuri tutahakikisha tunawaingiza kwenye time zetu
za taifa, tutawaendeleza, tutakuza vipaji vyao kwa maslahi  ya Serikali
zote mbili SMT na SMZ”. Amesisitiza Mhe, Mchengerwa.
Amewapongeza
kwa kuandaa mashindano hayo ambapo amefafanua kwamba dhamira ya
Serikali ni kuhakikisha kuwa inaandaa mashindano ya AFCON  2027 na
kusisitiza kuwa inawezekana iwapo kila  mdau atachukua wajibu wake.
Aidha,
amefafanua kuwa eneo la soka ndilo eneo pekee ambalo  linaweza 
kuwaunganisha watanzania wote bila kujali itikadi ya dini zao, rangi
wala  makabila yao.

 

 

 

    FacebookXGoogle+PinterestLinkedIn
PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO JULAI 5,2022
WAZIRI MKENDA ATETA NA WAZIRI WA ELIMU YA MSINGI WA AFRIKA KUSINI JIJINI DAR ES SALAAM

You may also like

Featured • Kitaifa

JWTZ YAKANUSHA TAARIFA ZA UONGO KUHUSU MAANDAMANO

Featured • Kitaifa

DKT MWIGULU APOKELEWA OFISI YA WAZIRI MKUU

Featured • Kitaifa

LATRA YAZINDUA TUZO KWA WATOA HUDUMA BORA ZA USAFIRI...

Featured • Kimataifa

RAIS RUTO APONGEZA UBUNIFU WA WAJASIRIAMALI WA...

Featured • Kitaifa

RAIS SAMIA AMTEUA DK.MWIGULU KUWA WAZIRI MKUU

Featured • Magazeti

PATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI...

About the author

Alex Sonna

View all posts

Copyright © 2025. Mzalendo Blog - Design by Yatosha Web Services.

  • Habari
  • Michezo
  • Burudani
  • Makala