Featured Kitaifa

WAZIRI MKENDA AWAPA KIBARUA VIONGOZI WAPYA WA SKAUTI TANZANIA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Skauti Tanzania na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda ,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika leo Julai 2,2022 Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Ali Abdulgulam Hussein,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika leo Julai 2,2022 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Omary Kipanga ,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika leo Julai 2,2022 Jijini Dodoma.

KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dk.hamis Mkanachi,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika leo Julai 2,2022 Jijini Dodoma.

Skauti Mkuu Mwantumu Mahiza,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika leo Julai 2,2022 Jijini Dodoma.
MDHAMINI wa Chama cha Skauti Tanzania Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika leo Julai 2,2022 Jijini Dodoma.
Baadhi ya Skauti Tanzania wakifuatilia hotuba ya Rais wa Skauti Tanzania Mhe.Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika leo julai 2,2022 jijini Dodoma.
Rais wa Skauti Tanzania na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof. Adolf Mkenda akipokea tuzo ya shukrani kwa niaba ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae ni mlezi wa Skauti Tanzaniawakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika leo julai 2,2022 jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda akionyesha Tuzo maalumu aliyotunukiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa malezi bora kwenye Chama Cha SKAUTI Tanzania iliyotolewa wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha SKAUTI Tanzania uliofanyika leo julai 2,2022 jijini Dodoma.
…………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda,amewataka viongozi wapya wa Skauti Tanzania kuimarisha Skauti shuleni na vyuoni ili kuondokana na changamoto ya malezi na ukatili wa kijinsia.

Hayo ameyasema leo Julai 2,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Chama cha Skauti Tanzania.

Amesema tabia nyingine zisizofaa ambazo watoto wanakuwa nazo zinasababishwa na kukosekana shughuli tofauti na za darasani ikiwemo michezo na mazoezi ya skauti.

“Tunahitaji kuimarisha malezi ya watoto wetu ili kuepuka utovu wa nidhamu utakaoweza kusababisha ukatili na unyanyasaji wa kijinsia shuleni,” amesema Prof. Mkenda.

Aidha Prof. Mkenda amewataka Skauti kuondoa migogoro na kuchagua viongozi waadilifu watakaoiongoza Skauti vizuri.

Amesema uchaguzi unaofanyika ambao ni wa wajumbe wa Bodi ya Skauti na majina matatu yatakayowasilishwa kwa Mhe Rais kuteua Skauti Mkuu ufungue ukurasa mpya wa utendaji na kwamba kazi kubwa iliyofanywa na viongozi waliotangulia isichafuliwe.

“Niwatake mkaoneshe uadilifu na nidhamu katika utendaji wenu mkiondoa kabisa migogoro iliyopo na kuhakikisha mnalinda jina la chama chetu hiki,” amesisitiza Prof. Mkenda.

 Kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amani wa Zanzibar, Naibu Waziri Mhe Ali Abdulgulam Hussein,amesema kuwa Skauti Zanzibar iko salama na inazidi kuimalika na kustawi na kuwa kwa mwaka 2021/22 wameweza kuongeza wanachama na kuzidi kuwa wamoja

Amesema kuwa  Zanzibar tayari imeshateua majina ya wajumbe ambao wataunda timu ya kusimamia mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Chama Cha Skauti ambayo yanafanyika ili kuzingatia maslahi ya Zanzibar na nafasi ya Zanzibar kwa Tanzania.

Awali  Skauti Mkuu, Mwantumu Mahiza amesema Skauti Tanzania imeweka mikakati ya kuondoa utegemezi na kwamba tayari wamepata eneo Jijini Dodoma ambalo litajengwa kambi ya Kimataifa ya Skauti, shule ya michezo, Chuo cha ufundi na kitega uchumi.

” Rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli aliahidi kutupa shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kujenga kituo hapa Dodoma kama tungepata hati na na kuwa na gharama halisi, na pia Rais Samia pia ametuahidi kutupa fedha kwa ajili ya jengo hilo.”

Kwa upande wake Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania Mhashamu Baba Askofu Gervas Nyaisonga,amesema kuwa wadhamini wa Skauti wamefarijika na kufurahi kuona Chama cha Skauti kinazidi kuwa na heshima, imara, kinaendelea kustawi na kuendelea vizuri huku Mali na Chama zikiwa salama mikononi mwa viongozi waadilifu.

About the author

mzalendoeditor