Baadhi ya washtakiwa wakishuka katika gari na kuingia katika jengo la kituo jumuishi cha utoaji haki kanda ya Arusha.
Jopo la mawakili wa utetezi wakijadili jambo katika chumba cha mahakama ya hakimu mkazi ndani ya kituo jumuishi cha utoaji haki kanda ya Arusha.
Wakili wa upande wa utetezi Jebra Kambole akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na kesi hiyo.
Wakili upande wa utetezi Peter Mandeleka akiongea na waandishi wa habari mahakamani hapo mara baada ya kesi hiyo kuhairishwa.
………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
25 kutoka tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakishtakiwa kwa makosa Mawili ikiwemo ya mauaji ya Askari Polisi na kupanga njama ya kuua.
Washtakiwa hao ni pamoja na Malongo Paschal, Albert Selembo, Simemeli Karongoi, Lekayoko Sirikoti, Sapati Parmwati,Ingoi Kanjwel, Sangau Ngimisi, Maorjoi Ngoisa, Morongeti Masako, Kambatai Lulu, Moloimeti Saing’eu, Ndirango Senge, Joel Lessonu, pamoja na Simon Olosikiria.
Washtakiwa wengine ni Damian Laiza, Methew Siloma, Luka Njausi, Taleng’o Leshoko, Kijoolu Olojoloji, Shengena Killed, Kelvin Nairoti, Lekernga Orodo , Fred Ledidi, Wilson Kilong pamoja na James Taki.
Kesi hiyo namba 11/2022 ambayo awali shtaka lilikuwa moja na leo Juni 30,2022 upande wa mashtaka wameiomba mahakama kuongeza shtaka lingine na kukubaliwa na mahakama ya hakimu mkazi chini hakimu Hariet Mhenga na kufanya mashtaka kuwa mawili ambapo shtaka la kwanza linalowakabili ni kupanga njama ya kuua siku na tarehe isiyofaahamika, maafisa wa serikali na askari waliokuwa wanafanya zoezi la uwekaji alama katika mipaka ya pori tengefu la Loliondo wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha.
Shtaka la pili Kudaiwa kufanya Mauji ya Askari Koplo Garlus Mwita namba G4200, katika Eneo la Selo Ololosokwan tarafa ya Loliondo Wilaya ya Ngorongoro tukio ambalo linadaiwa kutokea June 10,2022.
Hakimu Hariet Mhenga alisema kuwa mahakama ya hakimu mkazi haina mamlaka ya kuweza kusikilizwa shauri hilo ambapo kesi hiyo ipo mbele yake kwaajili ya upelezi lakini wanaruhusiwa kuongeza shtaka kwasababu hakuna sheria yoyote inayokataza mahakama hiyo kuongeza shtaka kama haitaleta athari katika mwenendo wa kesi.
“Kuongezeka kwa shtaka lingine halitaleta athari yoyote hivyo natupilia mbali pingamizi hili kutoka kwa mawakili wa utetezi kwani halina mashiko”Alisema.
Kesi hiyo inayoongozwa na wakili wa serikali Upendo Shemkole na utetezi wa jopo la mawakili 14 wakiongozwa na Jeremiah Mtobesya imehairishwa na kutajwa tena Julai 14, 2022 ambapo wakili wa serikali ameahidi kufikia tarehe hiyo upelelezi utakuwa umekamilika.
Wakili wa upande wa utetezi Peter Mandeleka akiongea na waandishi wa habari mahakamani hapo alisema kuwa kama timu ya utetezi Kuna mikakati waliyojiwekea ikiwemo kutoa changamoto kwanye shtaka la kwanza kwani shtaka hilo sio serious na kwamwajibu wa mabadiliko ya sheria mbalimbali mashtaka ambayo sio serious yakipelekwa mahakamani ni lazima upelezi wake uwe umekamilika.
Naye wakili Jebra Kambole alisema kuwa upande wa mashtaka wanatakiwa kukamilisha upelezi kwa haraka kwani kuna washtakiwa wenye changamoto za afya kutokana na uzee na mwanafunzi wa kidato cha tano ambaye anatakiwa kwenda shule hivyo upelezi ufanyike kwa haraka ili mwenye makosa ajulikane na asiye na kosa aachiwe huru akaendelee na shughuli zake.
“Kama kweli tuna nia ya kweli na Hawa watu tuhakikishe upelelezi unafanyika kwa wakati ili kama Kuna mtu mwenye makosa aonekane na kama kuna wasio makosa watoke wasiwe kama wanaonewa kwasababu hata wakionewa tutakuwa hatutendi haki kwa aliyekufa ni haki akakamatwa aliyetenda kosa kwahiyo maombi yetu ya msingi ni upelelezi ufanyike kwa haraka,” Alisema Kambole.