WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene,akizungumza leo Juni 29,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga. ,akizungumza wakati wa Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 lililofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 lililofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa,akizungumza wakati wa Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 lililofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma.
Mwenyekiti Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Bw.Ernest Kimaya ,akizungumza wakati wa Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 lililofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene, (hayupo pichani) wakati akifungua Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa lililofanyika leo Juni 29,2022 jijini Dodoma
…………………………………………
Na Eva Godwin-DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene amewataka watu wenye ulemavu kushirika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ili serikali iweze kupata takwimu zao ambazo zitakazoiwezesha kupanga mipango mbalimbali ya kimaendeleo kwa watu wenye ulemavu hapa nchini.
Simbachawene ametoa rai hiyo leo Juni 29,2022 jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Kuwajengea Uelewa Watu wenye Ulemavu kuhusu Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri Simbachawene amewasisitiza kushiriki zoezi hilo ili Serikali iweze kupata takwimu bora za watu wenye ulemavu.
“Mkusanyiko huu wa Watu wenye Ulemavu ni ushahidi wa Jitihada ya Serikali katika kuakikisha Wananchi wa Hali zote wanapewa fursa za kushiriki katika masuala yote yanayohusu maendeleo ya Nchi yetu”amesema
“Tunataka Ninyi muwe kipaumbele katika kushiriki na kuhamasisha Zoezi hili la Sensa ya Watu na makazi na tunatarajia kuona matokeo makubwa kutoka kwenu kwasababu Sensa ni ya Watu wote na hii itawaongezea ufahamu kuhusu zoezi hili”.amesema Waziri Simbachawene
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Athony Mtaka amesema mkoa wa Dodoma utahakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao za msingi katika mkoa huo ili kuimarisha ushiriki wao katika zoezi la Sense ya watu na makazi.
“Sisi kama Mkoa wa Dodoma tumeshaanza na tumekuwa na ushirikiano na viongozi wote wa vyama vya Watu wenye ulemavu Mkoa wa Dodoma kwenye shughuli zetu nyingi na kwenye hili tumefanya ushirikiano wa pamoja”amesema
” Mh. Simbachaweni nikuakikishie sisi kama Mkoa wa Dodoma tutatekeleza moja kwa moja maagizo utakayo toa siku hii ya leo”.amesema Mtaka
Naye Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa ,ameeleza kuwa ofisi ya taifa ya Takwimu imejipanga kuhakikisha wanachukua taarifa sahihi kwa walemavu
“Tumeweka maswali ya kutosha zaidi ya maswali kumi ambayo yatatusaidia kujua kwamba nani mlemavu wa aina gani,yuko wapi ,elimu yake,mahali anapoishi, analasirimali kiasi gani yote”amesema
” Hii ni kwa ajili ya kupata taarifa sahihi pamoja na kuisaidia Serikali kuweza kupanga mipango ya maendeleo”.amesema Dk. Chuwa
Mwenyekiti shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Ernest Kimaya amesema lengo la kongamano hilo ni kutoa elimu kwa watu wenye ulemavu ili kuwa nauelewa na kujua umuhimu wa sensa ya watu na makazi ili wahamasike kushiriki zoezi hilo.
“Sensa ya watu na makazi kwa upande wa Watu wenye Ulemavu Tanzania Bara na Zanzibar tukishirikiana na Tume ya Takwimu tumeboresha huongozo wa uboreshaji wa Makarani wa Sensa kwenye Dodoso la Jamii,Kaya na Majengo pamoja na maelezo yaliyojitosheleza kuhusiana na Walemavu
“Na sisi kama Watu wenye Ulemavu tutakuwa kipaumbele kuamasisha na kujitoa katika zoezi la Sensa Mwaka 2022”.amesema Kimaya.