Featured Kitaifa

IGP SIRRO ASKARI 156 WAFUKUZWA MAFUNZO

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wanafunzi wa kozi ya awali ya askari Polisi inayoendelea katika uwanja wa medani za kivita wilaya ya Siha, West Kilimanjaro katika shule ya Polisi Tanzania ambapo aliwataka wanafunzi hao kufuata sheria, kanuni na taratibu za shule hiyo ikiwa pamoja na kudumisha nidhamu ndani ya Jeshi la Polisi.

Baadhi ya wanafunzi wa kozi ya awali ya askari Polisi wakimuonesha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, moja ya zoezi la medani za kivita na namna wanavyoruka vikwazo mbalimbali wakiwa kwenye uwanja wa medani. Zoezi hilo limefanyika katika Shule ya Polisi Tanzania iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi

……………………………………….

Na Mwandishi Wetu-SIHA, KILIMANJARO

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema takribani askari Polisi wanafunzi 156 wamefukuzwa mafunzo ya kijeshi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo za utovu wa nidhamu na kufanya mambo ambayo hayakubaliki ndani ya shule ya Polisi.

IGP Sirro amesema hayo wakati alipofanya ziara kwenye uwanja wa medani za kivita wilaya ya Siha, West Kilimanjaro katika Shule ya Polisi Tanzania, ambapo pia amewaelekeza wanafunzi hao wa kozi ya awali ya askari Polisi kufuata sheria, kanuni na taratibu za shule hiyo ikiwa pamoja na kudumisha nidhamu ndani ya Jeshi la Polisi.

About the author

mzalendoeditor