Featured Michezo

WAZIRI BASHUNGWA AIPONGEZA YANGA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU YA NBC  2021/2022.

Written by mzalendoeditor

WAZIRI Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa ,akishuhudia mchezo kati ya Mbeya City na Yanga mechi iliyomalizaka kwa timu hizo kufungana bao 1-1 uwanja wa Sokoine Mbeya.

WAZIRI Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa,akikabidhiwa Kombe na  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa ajili ya kuwakabidhi Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara timu ya Yanga msimu wa 2021/22 katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

WAZIRI Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa,akimkabidhi  Kombe Nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto baada ya Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania  bara msimu wa 2021/22 katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

WAZIRI Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa,akiwavisha Medali wachezaji wa Yanga pamoja na benchi la Ufundi mara baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara  msimu wa 2021/22 katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

WACHEZAJI pamoja na Benchi la Ufundi la Yanga wakisherekea ubingwa wao mara baada ya kukabidhiwa rasmi kombe lao la ubingwa wa msimu wa 2021/22.

…………………………………..

Na OR TAMISEMI

WAZIRI Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa ameipongeza klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa 28 wa Ligi Kuu ya Tanzania bara kwa Msimu wa 2021/2022 unaowapa fursa ya kushiriki mashindano ya Klabu bingwa barani  Afrika.

Ametoa pongezi hizo Jleo Juni 25, 2022 Jijini Mbeya wakati akikabidhi kombe Yanga baada ya mchezo wao kati ya Mbeya city kumalizika kwa Sare ya kufungana bao 1-1 katika Uwanja wa Sokoine.

Waziri Bashungwa amewapongeza wachezaji wa Yanga,Viongozi pamoja na benchi la ufundi kwa kazi nzuri waliyoifanya mpaka kuchukua ubingwa huku wakiwa na mechi tatu mkononi.

”Nawapongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa 28 wa Ligi kuu mmepambana hadi mwisho hivyo nawaomba muanze maandalizi mapema ili mkaiwakilishe vyema nchi yetu katika Michuano ya Kimataifa kwenye Klabu Bingwa Afrika ambayo inatarajia kuanza September mwaka huu”amesema Waziri Bshungwa

Bashungwa  amempongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa za kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini kwa kasi ya kubwa na amekuwa akitoa miongozo, maelekezo, motisha na uwezeshaji mkubwa katika mchezo wa mpira wa miguu na sekta nzima.

Aidha  wito kwa wanamichezo kuendelea kujituma kwa kuwa michezo ni Ajira, kwasababu wachezaji huibuliwa na kuanzia ngazi za chini, Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kushirikiana na Wizara yenye dhamana ya michezo na wadau wengine kuhakikisha sekta ya michezo inasonga mbele.

 Bashungwa amevitaka vyama na vilabu vya michezo kushiriki katika michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA ili kupata vipaji vya kuendeleza sekta hii na kwa mashindano hayo ngazi ya wilaya na mikoa.

Vile vile, amempongeza Waziri mwenye dhamana ya michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais, ambapo ndani ya muda mfupi Tanzania imeweza kutwaa makombe  na kufuzu kwa kombe la Dunia kwa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu (Tembo worriors) litakalochezwa nchini Uturuki na timu ya wanawake  chini ya Umri wa miaka 17 (U17) Serengeti girls kule nchini India.

About the author

mzalendoeditor