Featured Michezo

SIMBA YAMUAGA WAWA KWA HESHIMA,YAIZAMISHA MTIBWA SUGAR LIGI YA NBC

Written by mzalendoeditor

MABINGWA wa Zamani wa Ligi Kuu  Simba wameendeleza mwendo wa kugawa dozi baada ya kuichapa mabao 2-0 Mtibwa Sugar mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huo pia umetumika kumuaga beki Kisiki Paschal Wawa ambaye anamaliza mkataba wake na Simba.

Mabao ya Simba yamefungwa na Pape Sakho dakika ya 17 na bao la pili limefungwa na Peter Banda akipokea pasi kutoka kwa Pape Sakho

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 60 wakiendelea kubaki nafasi ya pili huku Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya 12 kwa Pointi 32 kila timu ikiwa imecheza mechi 28.

About the author

mzalendoeditor