Featured Kitaifa

SERIKALI KUHAKIKISHA HUTUMA ZA UTAMBUZI WA UGONJWA WA SIKOSELI ZINAPATIKANA VITUO VYA AFYA IKIWEMO VIJIJINI.

Written by mzalendoeditor
Naibu katibu mkuu wa wizara ya Afya Dkt Seif Shekalaghe akiongea katika maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa Sikoseli duniania yaliyofanyika kitaifa mkoa wa Arusha.
 katikati ni naibu katibu mkuu wa wizara ya Afya Dkt Seif Shekalaghe akikata keki ya maadhimisho hayo kwa kushirikiana na watoto wenye ugonjwa wa Sikosel.
Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara ya Afya Dkt Omary Ubuguyu akiongea katika maadhimisho hayo.
Mmoja wa wagonjwa wa Sikoseli Sanyu Singa akiongea katika maadhimisho hayo.
Mtendaji mkuu wa Tanzania  Sikoseli alliance Dkt Deo Soka akiongea katika maadhimisho hayo.
Picha ya pamoja ya baadhi ya watumishi wa wizara ya Afya pamoja na watoto wenye ugonjwa wa Sikoseli.
……………………………………….
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Naibu katibu mkuu wa wizara ya Afya Dkt Seif Shekalaghe amesema kuwa serikali  kupitia wizara ya Afya imeingiza ugonjwa wa selimundo(Sikoseli) katika mpango mkakati wa kupambana na magonjwa yasiyoambukiza ili kuweza kupambana na ugonjwa huo ambao kila mwaka watu 11000 wanaozaliwa nao na  kumuagiza mkurugenzi wa tiba Dkt  Omary Ubuguyu kuhakikisha huduma za utambuzi sinapatikana katika vituo vya afya ikiwemo vijijini.
Dkt  Shekalaghe aliyasema hayo wakati akiongea kwa niaba ya Naibu waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel katika maadhimisho ya siku ya Selimundo Duniani  yaliyofanyika kitaifa mkoani Arusha ambapo alisema kuwa wameweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha wanapambana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuanzisha  cliniki katika hosipitali za wilaya, mikoa, Kanda na taifa hivyo muda umefika sasa wa kuweza kufika chini ili wagonjwa waweze kupata huduma kwa karibu.
“Turudi wizarani  na kuhakikisha kuwa tukiandhimisha siku hii mwaka ujao wagonjwa hawa hawaji na changamoto ya umbali mrefu kufikia cliniki za Sikoseli lakini pia NHF kuhakikisha kuwa katika vile vitita huduma hizi ziingizwe katika bima ya Afya ili waweze kupata huduma hii vizuri kwasababu huu ni ugonjwa ambao wagonjwa hawa wanaishi nao maisha yao yote,” Alisema.
“Nchi yetu ni nchi ya tano Duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wenye Sikoseli ambapo kila mwaka wanaozaliwa watu elfu kumi na moja na mpaka Sasa idadi ya watu wenye siko seli ni ni laki mbili  ambapo watu watano mpaka saba  kati ya mia moja waliopo chini ya miaka mitano hufa kwasababu mbalimbali kutokana na madhara yanayosababishwa na Sikoseli,” Alisema Dkt Shekalaghe.
Alisema  kuwa kwasababu ipo katika mikakati watahakikisha inaenda kwenye ngazi za chini Ili huduma hiyo ya utambuzi iweze kupatikana Kwenye maeneo mengi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maabara ambapo mikakati hiyo itasaidia wagonjwa kupata tiba tofauti na ilivyokuwa mwanzoni kwasababu zipo dawa.
Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt Silvier Mamkwe aliitaka jamii kuondoa Mila potofu juu ya ugonjwa wa Sikoseli badala yake wazingatie kufanya vipimo wakati wa kupata wenza ili kuepuka kuoana wote wakiwa na vina Saba vinavyofanana hali itakayosaidia kutozaa watoto wenye ugonjwa huo.
“Huwezi kujijua kama una ugonjwa huu bila kupima hivyo tukate hii cheni ya kuendelea kurithi kwa kupima, kwani serikali peke yake haiwezi ni muhimu tukashirikiana kumaliza,” Alisema.
Naye mtendaji mkuu wa Tasisi ya Tanzania Sikoseli  alliance Dkt Deo Soka alisema kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha huduma za Sikoseli zinaboreshwa ambapo wameweza kuongeza uelewa wa ugonjwa huo kwa wananchi, wametengeneza miongozo ya matibabu pamoja na kuwezesha kuingizwa kwa dawa muhimu za ugonjwa huo.
“ Kwasasa tunataka kuelekea katika suala la kuzuia kwasababu tumeona ni muhimu zaidi kujikita katika kuzuia kuliko kukaa tukisubiri kuja kutibu,” Alisema Dkt Soka.
Mmoja wa mashujaa wa Sikoseli ambaye ameishi na ugonjwa huo mwaka wa 44 sasa na kuweza pia kupata mtoto Sanyu Singa alisema kuwa wao kama mashujaa wanakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa ni elimu juu ya Sikoseli kutokuwepo katika jamii.
“Tunatamani elimu itolewe kwanzia majumbani ili tunaoishi nao weweze kutuelewa na wajue kuwa ugonjwa huu hauambukizwi kwa kugusana bali ni wakurithi lakini pia mtusaidie clinic ziwepo maeneo yote ikiwemo vijijini,” Alisema.

About the author

mzalendoeditor