Featured Michezo

TANZANIA NA INDIA KUJA NA MAPINDUZI MAKUBWA KWENYE UTAMADUNI

Written by mzalendoeditor

 

Na John Mapepele.
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema  kuwa
Tanzania na India zinakwenda kupitia na kuboresha mikataba ya
mashirikiano ya awali  kwenye eneo la Utamaduni na Sanaa iliyojiwekea 
mwaka 1984 ili  kuiboresha iweze kuleta mapinduzi makubwa na ya haraka
kwa faida ya pande zote.
Mhe,
Mchengerwa ameyasema haya leo Juni 17, 2022 akiwa na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Dk. Hassan Abbasi wakati alipotembelewa ofisini kwake na
Balozi wa India nchini Mhe.  Binaya Srikanta Pradhan na kufanya
mazungumzo ya kuendeleza mashirikiano kwenye sekta hizo.
Aidha,
amesema mambo mengi yalikubalika   baina ya nchi zote mbili hususan 
kuendelea kwa tamaduni  pia  kumekuwa na mambo mengi ambayo yameandikwa
ambayo kuna haja ya kufanya mapitio.
Ameongeza 
kuwa katika maongezi hao  wamekubaliana kuwa  na kituo maalum cha
kuandaa filamu ambacho kitatumika kwa nchi za Afrika mashariki ambapo 
baadhi ya wasanii kutoka India  watashiriki moja kwa moja kwenye eneo
hili.
Pia
amesema eneo jingine  kubwa ambalo wamejadili  ni kuhusu umuhimu wa  wa
kufanya mkutano mkubwa kuhusu bahari ya Hindi ambao utajumuisha nchi
hizo  mbili.
Amesema tamasha hilo litasaidia kuonyesha historia za nchi zote zilikotoka zilipo na zinakoelekea
Aidha,
amesema  bahari ya Hindi imebeba historia kubwa ambayo tayari watafiti
kutokana  India na Tanzania wamefanya utafiti hivyo ni muhimu  kuutumia
utafiti huo kwa faida ya nchi zote.
Naye 
Mtaalam  na Mtafiti  Arindam Mukherjee ambaye ameambatana  na Mhe.
Balozi amefafanua kuwa tafiti zinaonesha kuwa  Bahari ya Hindi ilikuws
ikitumika kwa miaka mingi kufanya biashara  ambapo yapo baadhi ya maeneo
ambayo yamethibitika yamekuwa yakikaliwa na waswahili na pia kumekuwa
na mfanano wa maneno ya kiswahili.

About the author

mzalendoeditor